Mungu uwe upande wetu
Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mara tu baada ya tukio hilo
eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....Eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu  kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....


Na Ahmed mahmoud wa Globu ya Jamii, Arusha
MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmoja yu  mahututi na wengine zaidi ya 49  wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka kitu kinachosadikiwa ni bomu majira ya saa  4 asubuhi leo  wakati wa sherehe za ufunguzi  wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.


Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisco  Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat  lebulu,  na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.

Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za  maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina  Fredirik, Joram  kisera, Novelt  John, Rose  pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt  John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .

Wengine ni Rioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim 

Mkuu wa mkoa wa  Arusha, Magesa Mulongo ,  ameagiza vyombo vya ulinzi na  usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.

Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
Umati wa  wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo.
 Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja  amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
Picha kwa hisani kubwa ya 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2013

    Jamani Tanzania tunaelekea wapi? Tumefikia hatua ya kulipuana mabomu ibadani? Makanisa yanakuwa si sehemu salama? Iwapi amani ya nchi yetu? Kiwapi kisiwa cha amani? Tusipobadilika tutafikia pabaya!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2013

    Nafikiri vyombo vya usalama vikae macho na FALSE-FLAG TERROR. Nchi inapita kwenye msukosuko. Nashauri wafuatilie mawasiliano ya aina yote; hata ya wale wote wanaofanya kazi katika kanisa hilo. Pili kama kuna security camera waangalie picha zote. Tatu wachukue finger prints pia za mabaki ya bomu hilo na wajaribu kufuatilia chanzo cha bomu. Tanzania mambo hayo ni ABNORMAL sana. Tuwe macho Watanzania wenzangu; wakubwa wanataka mali zetu (gesi,mafuta,uranium,dhahabu,copper,n.k.). Muumba atulinde na lililo na shari na Ailinde nchi yetu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2013

    Taratibu tunaanza kuvuka mistari sasa."FBI" yetu ,tatizo inatumia muda mwingi kwenye siasa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2013

    Hili ni jambo la kusikitisha sana, mlipuko kanisani.....tafadhali tusaidie kupata taarifa za kina kadiri itakavyowezekana?!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2013

    Jamani Watanzani tunaelekea wapi? Sasa ibada zifanyikie wapi? poleni sana Ndugu zangu wangu wa Arusha Mungu awasaidie majeruhi wapone haraka.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2013

    mimi nawasiwasi yaani haya mambo yanakuja wakati wasasa kuna mafuta gasi????watzanzani hatuna tabia yakulipuna kinyama hawa ni watu wa njee washenzi wanataka kutuharibia amani kwa damu walizo fanya kwingine.

    ReplyDelete
  7. Tunawaombea wote walioathirika
    Na mlipuko huo

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2013

    Poleni sana ndugu waamini

    ReplyDelete
  9. Inauma sana poleni watanzania wenzetu huko mungu awasaidie wate mlioathirila na tukio hilo.......sasa wataanza kuingiza mambo ya siaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 05, 2013

      Poleni sana ndugu zetu tuko pamoja

      Delete
  10. AnonymousMay 05, 2013

    Poleni sana wana Arusha na Watanzania kwa ujumla. Tunawaombea majeuhi wapate wapone haraka!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 05, 2013

    Arusha juzi juzi tu vurugu za chuo kimefungwa na sasa ni hii skendo mbaya mno. Hivi Tz kila mtu anaishi na bomu ndani? Hivi hii ni Palestina au?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2013

    Poleni sana kwa mliopata janga hilo .mungu atajidhihirisha

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2013

    Huu ni wakati wa Viongozi wa dini kuomba Mungu kuliko wakati mwingine wowote katika miito yao. wanatakiwa kuwaongoza waumini wao kumuomba Mungu kwa bidii ili Mungu awe karibu na kazi yake kuliko awali. Hali haitabiriki shetani yupo kazini siku hizi za mwisho ana hasira

    Kwa hiyo, badala ya viongozi wa dini kutumia muda mwingi katika siasa na masuala mengine, watumie muda mwingi katika kujificha kwenye maombi

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 05, 2013

    Ikowapi amani yetu ndugu watanzania? Tumuombe Mungu ataepushe na balaa la udini.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 05, 2013

    Serikali lazma iwekeze hata kwa kutumia wataalamu wa scotland police kupata chanzo cha bomu na walioshiriki kwenye vitendo hivi viovu vya uvunjifu wa amani. Watanzania tushikamane na tupendane sana,tuache hisia ila adui yetu tumtafute wote kama watanzania. Utengano usiwepo kati yetu kwa kipindi hichi. Lazma tuzishinde nguvu za wanataka watanzania wasiwe na amani. Serikali tusaidieni kuwapata wachochezi na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi hii ili tupange na tufaidi wote na kwa amani utajiri wa mali zetu asili alizotupa Mungu. Umoja ni nguvu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...