Majeruhi wa Mlipuko huo akipata huduma ya kwanza mara tu baada ya tukio hilo
Na Ahmed mahmoud wa Globu ya Jamii, Arusha
MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmoja yu mahututi na wengine zaidi ya 49 wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka kitu kinachosadikiwa ni bomu majira ya saa 4 asubuhi leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.
Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisco Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat lebulu, na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.
Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina Fredirik, Joram kisera, Novelt John, Rose pius, John James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, .
Wengine ni Rioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo , ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.

Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka

Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
Umati wa wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo. Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
Umati wa wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo. Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.
Picha kwa hisani kubwa ya






Jamani Tanzania tunaelekea wapi? Tumefikia hatua ya kulipuana mabomu ibadani? Makanisa yanakuwa si sehemu salama? Iwapi amani ya nchi yetu? Kiwapi kisiwa cha amani? Tusipobadilika tutafikia pabaya!!
ReplyDeleteNafikiri vyombo vya usalama vikae macho na FALSE-FLAG TERROR. Nchi inapita kwenye msukosuko. Nashauri wafuatilie mawasiliano ya aina yote; hata ya wale wote wanaofanya kazi katika kanisa hilo. Pili kama kuna security camera waangalie picha zote. Tatu wachukue finger prints pia za mabaki ya bomu hilo na wajaribu kufuatilia chanzo cha bomu. Tanzania mambo hayo ni ABNORMAL sana. Tuwe macho Watanzania wenzangu; wakubwa wanataka mali zetu (gesi,mafuta,uranium,dhahabu,copper,n.k.). Muumba atulinde na lililo na shari na Ailinde nchi yetu
ReplyDeleteTaratibu tunaanza kuvuka mistari sasa."FBI" yetu ,tatizo inatumia muda mwingi kwenye siasa.
ReplyDeleteHili ni jambo la kusikitisha sana, mlipuko kanisani.....tafadhali tusaidie kupata taarifa za kina kadiri itakavyowezekana?!
ReplyDeleteJamani Watanzani tunaelekea wapi? Sasa ibada zifanyikie wapi? poleni sana Ndugu zangu wangu wa Arusha Mungu awasaidie majeruhi wapone haraka.
ReplyDeletemimi nawasiwasi yaani haya mambo yanakuja wakati wasasa kuna mafuta gasi????watzanzani hatuna tabia yakulipuna kinyama hawa ni watu wa njee washenzi wanataka kutuharibia amani kwa damu walizo fanya kwingine.
ReplyDeleteTunawaombea wote walioathirika
ReplyDeleteNa mlipuko huo
Poleni sana ndugu waamini
ReplyDeleteInauma sana poleni watanzania wenzetu huko mungu awasaidie wate mlioathirila na tukio hilo.......sasa wataanza kuingiza mambo ya siaaa
ReplyDeletePoleni sana ndugu zetu tuko pamoja
DeletePoleni sana wana Arusha na Watanzania kwa ujumla. Tunawaombea majeuhi wapate wapone haraka!
ReplyDeleteArusha juzi juzi tu vurugu za chuo kimefungwa na sasa ni hii skendo mbaya mno. Hivi Tz kila mtu anaishi na bomu ndani? Hivi hii ni Palestina au?
ReplyDeletePoleni sana kwa mliopata janga hilo .mungu atajidhihirisha
ReplyDeleteHuu ni wakati wa Viongozi wa dini kuomba Mungu kuliko wakati mwingine wowote katika miito yao. wanatakiwa kuwaongoza waumini wao kumuomba Mungu kwa bidii ili Mungu awe karibu na kazi yake kuliko awali. Hali haitabiriki shetani yupo kazini siku hizi za mwisho ana hasira
ReplyDeleteKwa hiyo, badala ya viongozi wa dini kutumia muda mwingi katika siasa na masuala mengine, watumie muda mwingi katika kujificha kwenye maombi
Ikowapi amani yetu ndugu watanzania? Tumuombe Mungu ataepushe na balaa la udini.
ReplyDeleteSerikali lazma iwekeze hata kwa kutumia wataalamu wa scotland police kupata chanzo cha bomu na walioshiriki kwenye vitendo hivi viovu vya uvunjifu wa amani. Watanzania tushikamane na tupendane sana,tuache hisia ila adui yetu tumtafute wote kama watanzania. Utengano usiwepo kati yetu kwa kipindi hichi. Lazma tuzishinde nguvu za wanataka watanzania wasiwe na amani. Serikali tusaidieni kuwapata wachochezi na wanaotaka kuvuruga amani ya nchi hii ili tupange na tufaidi wote na kwa amani utajiri wa mali zetu asili alizotupa Mungu. Umoja ni nguvu.
ReplyDelete