Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.

Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo,chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2013

    Mwangalie yule jamaa mmoja hapo anacheka. Hujui jamaa ana watoto au vipi, nini kimemsibu. Nyani haoni kundule!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2013

    No premise/s are provided to support the stated conclusion kwamba kajirusha! Labda kasukumwa!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2013

    Kuna uhakika gani kwamba kajirusha??

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2013

    inasikitisha sana.. je alikua mwenyewe hotelini hapo..

    ReplyDelete
  5. What. A sad way to lose ones life.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2013

    Mungu anusuru roho yake,so sad.kwa familia na ndugu na jamaa wa karibu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2013

    UCHUNGUZI UFANYIKE KWA MAKINI SANA. UNAWEZA SEMA KAJIRUSHA MWENYEWE KUMBE KARUSHWA TOKA JUU. WANAUSALAMA TUNAWAACHIA KAZI YAO. WAFUATILIE MAZUNGUMZO YA KWENYE SIMU KWA SIKU ZA NYUMA PIA NA AINA NYINGINE YEYOTE YA MAWASILIANO ALIYOKUWA AMEYAFANYA. NA WAENDELEE NA UCHUNGUZI ZAIDI YA HAPO; CHA MSINGI KUJIRIDHISHA KAMA ILIKUWA NI AJALI YA KAWAIDA AU AMEJIUA MWENYEWE AU KITU KINGINE CHOCHOTE. HII ITASAIDIA KULINDA USALAMA WA WATANZANIA NA WAGENI. KAZI NJEMA

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2013

    kwani akiwe na meno nje amecheka...kucheka ni mpaka kutoa sauti....kutabasamu ni kuonesha ishara ya furaha bila ya kucheka........

    la muhemu ni marehemu inisikitisha sana habari hiyo...lakini mwandishi si inawezekana pia ameuawa, yaani mtu amemsukuma kutoka juu?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2013

    Bongo Bwana. hamna mtu anamwangalia kama anahema au kumpa msaada wowote. Nakumbuka kama jana mzazi wangu marehemu alipata mstuko wa moyo na hamna hata dakrari mmoja Muhimbili aliyemsaidia tulipofika mpaka Daktari wa Kichina kamwona katika benchi na moja kwa moja alijua kuwa anahitaji matibabu ya haraka.
    Maisha ya Binadamu Afrika hayana thamani.Halafu tunashangaa kwa nini Waafrika tuna maisha mafupi kuliko wenzetu. Mimi nitakufa hapa hapa ughaibuni wala sitaki hata maiti yangu irudi Afrika.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2013

    Hii ndio Tz bana na wengine wako bize na simu kupata picha za kupost Facebook, Twitter, etc lakini sio kuokoa kabisa. Huu utandawazi umetuathiri sana. Nilishuhudia pia kwenye ghorofa liloanguka hivi karibuni watu wako bize na vikamera bila ya kusaidia shughuli za uokoaji. Huku tunakoelekea siko kabisa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2013

    anonymous wa mwisho umesema kweli na nakuunga mkono lakini kidogo pia nataka kukupa hizi data, hata huko ughaibuni kuna ubaghuzi wa ngozi zetu nyeusi usisikiye na weusi sisi wa kiafrica pia weusi wa huko huwa hawatupendi kama tulivyodhani kwamba watatupenda. ni mpango umepangwa zamani kwamba weusi tusipendane na kusikilizana na tusipate maendeleo unadhani wanataka bara la africa litajirike no and no wanataka kila siku tuwe hivi hivi aminiya na fanya uchunguzi kama unaniona muongo utayaona mambo

    jiulize jambo mmoja tu hizi simu za mikono kwa nini zije africa kwa sana utasema maendeleo lakini chunguza na uzazi wampango kama vile sisi wanyama tunazaa ovyoo eti hatujui uzazi wa mpango chunguza utaona yani wee acha tuu mambo kibao ila tumuombe mungu tutafika na tanzania yetu na africa yetu mungu tukimuabudu mungu ipasavyoo

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 04, 2013

      Out of topic...comment yako haiendani na story iliyoandikwa hapo juu. Jaribu tena..

      Delete
  12. AnonymousMay 03, 2013

    Nilidhani stress ziko majuu tu kumbe hata home labda kweli jamaa kajirusha kwa madeni anadaiwa au labda kweli jamaa kasukumbwa who knows tungekuwa na forensic scientist tungeyajua haya yote siyo eti polisi tu waje na kufanya uchunguzi hatuna taalumu hii ya juu so cha kufanya si kulaumu nchi yetu wala vyombo vyetu cha kufanya kwa kila mtanzania aliye majuu yes nasema tena kwa kila mtanzania aliye majuu akiwa mbara au mwana kisiwani akiwa majuu anapiga box afanye juu chini apate makaratasi na aende kusoma siyo kujiachia piga box na usome hata trade school nendeni babaaa na maaaa mje msaidiye nchi yenu na ujuzi wenu hata wa trade school siyo kujiachia na kujiweka huko eti siji tena africa na usije mkata kwao mtumwa hata kama kuna maisha mabaya huko kumbuka si kwenu kuna siku uta pa miss kwenu au utafukuzwa urudi kwenu KIBUYU USHUZI hapo ndo utajua nini summer time au winter time ukishafika airport ya kwenu bongo land,visiwani island

    kazi kweli ipo tutafika lakini mungu ibariki africa na watu wake wote tuwe wamoja united africa kama they will let us, because iam sure they will not let us

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 03, 2013

    hakuna mtu anayeweza kujirusha for no reason labda kichaa labda unaweza kuta kasukumwa au kuna kitu kilikua kinamsumbua

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 03, 2013

    Bwana Ebrahim Dhala umesema la ukweli kabisa.

    Kaka Michuzi, chonde chonde iondoe picha hiyo, kama ni habari tushaipata. Hii ni kwa ajili yawatoto wake, ndugu wa karibu, jamaa na marafiki wanaomjua huyu mhanga wa tukio. Inawazidishia machungu zaidi. Hata kiungwana tu inatia uchungu bila hata kuiona picha yenyewe. Ahsante.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2013

    Anony wa kumi na moja toka juu umepasua jipu

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2013

    Jamani Mungu amsaidie huwezi juwa nini kimempata baba wa watu jamani, Maisha yana changamoto nyingi sana! Tuachie uchunguzi wa polisi au wanausalama itajulikana kama alijitupa mwenyewe au la!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2013

    Siri ya mtu ni kichaka!

    Hatuwezi kujua kwa undani ni nini kimemsibu ndugu Shirima hadi yakamfika hayo.

    ReplyDelete
  18. Topic ya ubaguzi wa rangi haihusiani na picha na habari yake

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 07, 2013

    INAHUSU MKUU UNGESOMA VEMA UNGEJUA KWA NINI NIMEANDIKA VILE KUNA MTU AMESEMA HAJI TENA TANZANIA ETI KISA MZAZI WAKE MUHIMBILI HAJAANGALIWA MPAKA AKAJA MCHINA KUMUANGALIA NDUGU YAKE YEYE ATABAKI MAJUU SO NIMEMJIBU ASIWE ASIWE NA DHANA NA FIKRA HIZO KWAMBA ETI AKIWA HUKO MAJUU NDO ANA ENJOY LIVE NA KULA KUKU KUMBE HATA SIKU MMOJA HAJAWAHI KUZUNGUMZA ANA KWA ANA NA KUNYWA BAI PAMOJA NA MZUNGU ANAYE FANYA NAYE KAZI

    SO SOMA VIZURI USIJE HAPA KATIMA BLOG UJIJIFANYA MJANJA KIDUME MBEGU KUMBE MCHICHA WA BINTI MARINGO

    SOMA TOPIC VIZURI IFUATILIYE VIZURI USIDHANI TUNAROPOKA OVYO WENZAKO SHULE IMEPANDA HAPA USICHEZE NA WATU USIO WAJUA NA KUWA LIBUKENI WAKUJIBU BILA KUTAFAKARI

    WEWE MUME IAM ANSWERING TO YOU

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 07, 2013

    inahusu mkuu mume ubaguzi upo na lazima tuu seme kuna mtu yupo majuu anasema haji tsna tanzania kisa hakuna huduma njema umemsoma huyu anonymous usije hapa kifua cha nazi ujajititimua na wewe uonekana umechangia kidume cha mchele wa mahenge

    kabla hujaingia humu ujuwe kuna waliokwenda shule wanajua kuchambua mada na kujibu na kutoa michango yao siyo wewe unakuja hapa na kujifanya mjuaji kumbe juhaa mkubwaaa

    soma usomekeee

    Anonymous said...
    Bongo Bwana. hamna mtu anamwangalia kama anahema au kumpa msaada wowote. Nakumbuka kama jana mzazi wangu marehemu alipata mstuko wa moyo na hamna hata dakrari mmoja Muhimbili aliyemsaidia tulipofika mpaka Daktari wa Kichina kamwona katika benchi na moja kwa moja alijua kuwa anahitaji matibabu ya haraka.
    Maisha ya Binadamu Afrika hayana thamani.Halafu tunashangaa kwa nini Waafrika tuna maisha mafupi kuliko wenzetu. Mimi nitakufa hapa hapa ughaibuni wala sitaki hata maiti yangu irudi Afrika.

    May 03, 2013

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...