Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ufukwe wa Coco beach wakati wa Tamasha la Cheka Nao lilioandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Wafanyakazi mei mosi juzi jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma baba ya muziki Romarii Mng'anda akiwaongoza waimbaji wenzake wakati wa tamasha la ChekaNao liliandaliwa na Vodacom Tanzania ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi hapo juzi na kufanyika katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa Kikundi cha wakali dansi wakionyesha ukali wao wakati wa onyesho la Cheka Nao liliandaliwa na Vodacom Tanzania katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam,Ikiwa ni sehemu ya Kusherehekea sikukuu ya Mei mosi hapo juzi .
Msanii anaechipukia wa Kizazi kipya Dogo Lila toka kundi la TMK Wanaume Halisi akionyesha umahiri wake wakati alipokuwa akiimba kwenye Tamasha la Cheka Nao lililoandaliwa na Vodacom Tanzania katika ufukwe wa Coco Beach jijjni Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi hapo juzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2013

    ebwana eeh dogo kaniacha hoi kwa mavazi yake utadhani mnyamwezi ha ha ha dogo shule bwana najua unatakuta risiki lakini na huku pia shule dogo usiache shule

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2013

    Mwambie na hao wanaomkenulia wajue wanamlostisha dogo, si unajua wabongo wengi hupendaga zaidi nonsense kuliko sense

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...