Mganga wa jadi Aweso Kipaku ambaye ni diwani wa kata ya Mswaha iliyopo wilayani Korogwe, akiwa ameshikilia kitu kinachodaiwa ni jini alilolitoa katika moja ya darasa la shule ya msingi Kwemsala iliyopo kata ya Mtindiro wilayani Muheza juzi, wengine aliyevaa fulana ya punda milia ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Shabani Hamisi.
Na Mashaka Mhando,Muheza

DIWANI wa kata ya Mswaha iliyopo wilayani Korogwe, Aweso Kipaku amefanya kazi ya kuwanusuru wanafunzi wa shule ya msingi Kwemsala iliyopo kata ya Mtindiro wilayani Muheza, waliokuwa wakianguka kutokana na kuwepo madai ya imani za kishirikina.

Akifanya kazi hiyo, juzi katika shule hiyo Diwani huyo aliyealikwa na kamati ya shule ya kijiji hicho, alianza kupita kila darasa la shule hiyo huku akionekana amepandisha mapepo yaliyokuwa yakimuongoza huku wananchi wa kijiji hicho wakijazana kuona kazi anayofanya diwani huyo.

Diwani huyo mara baada ya kukimbizana na vitu vilivyokuwa havionekani kwa macho, alipoingia kwenye ofisi inayokaliwa na walimu, alipiga kelele kutaka aletewe unga wa sembe, maji na kuku alipopata vitu hivyo, aliibuka na pembe kubwa iliyokuwa imefungwa vitambaa vyeupe na vyekundu.

"Wananchi hivi vitu vilivyotoa mnavyoviona ndivyo vilivyokuwa vikiwasumbua wanafunzi, lakini jini jingine kubwa limekimbia huko katika makazi...Kazi ya kupambana nalo nitaifanya kesho (Ijumaa iliyopita)," alisema diwani huyo huku akiwa amekishika mkononi.

Akizungumza na wananchi mara baada ya diwani huyo kutoa vitu hivyo, Mwenyekiti wa kamati ya shule Shaban Hamis alisema tatizo la wanafunzi kuanguka katika shule hiyo lilianza tangu mwaka juzi na walipoitisha mkutano wa kijiji, viongozi wa dini walisema wangefanya maombi kuwanusuru watoto hao, lakini hawakuweza kufanya maombi hayo.

"Tuliona watoto wetu wanaendelea kuanguka wakipelekwa hospitali wanelezwa wana matatizo ya kisaikolojia, lakini tukiwapeleka kwa waganga wa kienyeji wanatibiwa na kupona, tukaona ni vema tumlete mganga huyu Kipaku (Diwani) ili awanusuru watoto wetu," alisema mwenyekiti huyo.

Mwalimu mmoja shuleni hayo Sophia Msangeni, alisema tatizo la wanafunzi kuanguka limekuwa likisababisha kushuka kwa taaluma shuleni hapo hatua ambayo ilikuwa ikileta kero na usumbufu mkubwa mara inapotokea suala la watoto kuanguka ambapo kwa siku wanaanguka watoto 20.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2013

    mabo hayo magumu kuelewa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2013

    Haya mambo yapo sana katika jamii zetu.

    Nini kifanyike?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2013

    Nadhani taaluma ndiyo itashuka kabisa kwa mtindo huu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2013

    ooo hooo TZ kwisha serikali haina issue za kishirikina.huyo kaweka mbwembwe zake hapo shule ili ajinadi vizuri kwakweli nchi yetu bado iko diza nene sana.hii jamii ndo ilete maendeleo kweli?nyambafu

    ReplyDelete
  5. Al MusomaMay 17, 2013

    Naye sasa hivi atagombea ubunge. Ya Rabi tunusuru!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 18, 2013

    Je vipi au ni tangazo la vifaa vya NIKE?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 18, 2013

    Nchi yetu imebarikiwa sana kuwa na watalamu kama hawa. Kwanini tunashindwa kuuza utalamu huu nchi za magharibi ili kupata fedha za kigeni?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 18, 2013

    Hiyo ya kudai sembe na Kuku !! Mhhhhh! Hii kali? Mie mbavu sina!!! Hizi njaa zitaleta mengi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 18, 2013

    Tanzania tunashabikia sana huu ujinga!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 18, 2013

    Ha ha ha haaa aaaah haki ya Mungu

    ReplyDelete
  11. tangu lini JINI akawa hivyo au akaonekana? Huyu Diwani akamatwe kwani inaonekana yeye ndie kaweka kwa ajili ya kujipandisha chart!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 18, 2013

    KAMA DIWANI NI MSHIRIKINA UNAFIKIRI NCHI ITAKUWA KATIKA HALI GANI?UPUMBAVU MTUPU

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 18, 2013

    Mbinu za waganga hizo kudanganya watu. Wanaweka wenyewe hayo mauzauza ili muwatafute then muwalipe. Aliposema kakimbia, ni kutaka picha iwe na party two na gharama zaidi.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 18, 2013

    Kweli duniani kuna mambo.
    Ukistaajabu ya Musa hakika na ya Firauni utayaona.
    Ee Mungu tunusuru.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 18, 2013

    Huyo mganga anaonekana Kama mshabiki wa Arsenal, kwa nini asiwasaidie ili wapate hata Kombe moja msimu ujao?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 18, 2013

    Metaphysical. Ha ha haaa!! Sitake ncheke mie!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 18, 2013

    Hapa tunahangaika Makal ya WANYAMA PORI HAPO JUU KUWA TEMBO WANAUWAWA NA MAJANGILI.

    SASA KAMA KIONGOZI MHE. DIWANI ANAO UWEZO WA KISAYANSI KWA NINI ASIISAIDIE TANZANIA KUKABILIANA NA MAJANGILI NA KUOKOA MAUJAI YA TEMBO?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 18, 2013

    Mwanasayansi Albert Einstein aliwahi kuandika hivi:

    ''I fear that day when man exceeds uses of science and Technology, mankind will be totally confused''

    ...YAANI ''NINAOGOPA ITAKAPOFIKA SIKU MWANAADAMU AKITUMIA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUPITA KIASI, MWANADAMU ATAKUWA MAECHANGANYIKIWA''

    Ndio hapa sasa yanajiri huko Wilayani Korogwe!

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 18, 2013

      Hawa waganga ukiwaangalia ni kama matahira kuanzia yule babu wa kikombe kule loliondo cha ajabu wabongo wengi bado wanamini hiyo danganyatoto ya mwaka 47 ndio maama wabunge mawazili walienda loliondo kunywa kikombe cha maji ya uzima wala usishangae huyo anafukuzana na kimvuli chakemwenyewe halafu anasema jini

      Delete
  19. AnonymousMay 18, 2013

    ujinga mtupu...sio vigumu kuona poda usoni mwa huyo "mganga" ni sawa sawa na poda ya "jini". Basi mazingaombwe nayo ni kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...