Wapenzi wetu wa Staki Shari, Tunapenda kuwafahamisha kwamba timu yenu ya Golden Bush imethibitisha kushiriki katika Bonanza ya tarehe 19/05/2013 litakalo fanyika katika viwanja vya Staki Shari. Golden Bush itakuja na kikosi kamili kama kinavyoonekana katika picha hapo chini.  

Golden Bush itaingia uwanjani mnamo saa mbili kamili asubuhi tayari kutoa kipigo stahiki kwa timu yoyote itakayopambana na sisi. Waandaaji wa mashindano wanatambua ubora wa Golden bush itakoyokuwa ikiongozwa na nahodha wake Wisdom Ndlovu, hivyo tunategemea kupangiwa timu itakayoonyesha upinzani na kuleta burudani kwa mashabiki watakaokuja kushuhudia Bonanza hilo.
Tungependa kuwataarifu kwamba mchezaji wa zamani wa yanga na timu ya taifa ya Tanzania Salum Athuman Mbududu amesajiliwa rasmi baada ya kufuzu majaribio ya wiki moja, hivyo tunapenda kumtangaza kuwa kuanzia leo Salum Athuman atakuwa mchezaj halali wa Golden bush Veterans.

Imetolewa na msemaji wa timu
Onesmo Waziri "Ticotico"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...