Waziri wa Fedha na Uchumi Mhe Dk. Wiliam Mgimwa akitiliana saini na Balozi wa EU Mhe. Filiberto Sebregondi.

Na Frank Mvungi na Eleuteri Mangi-MAELEZO

SERIKALI ya Tanzania imetiliana saini mkataba na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Ulaya( EU) utakaowezesha Tanzania kupatiwa shilingi bilioni 20 kusaidia maendeleo katika sekta ya kilimo cha miwa kwa wakulima wa Visiwa vya Zanzibar.

Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam kati ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mhe Dk. Wiliam Mgimwa na Balozi wa EU Mhe. Filiberto Sebregondi, ambapo unategemewa kuisaidia serikali katika kuondoa umasikini kwa wananchi wake na kuiwezesha nchi kupiga hatua ya maendeleo kupitia sekta ya kilimo.

Waziri Mgimwa alisema kuwa msaada huo pia utasaidia kuwajengea wananchi uwezo wa kutekeleza kilimo chenye tija na kupanua soko la bidhaa zitokanazo na miwa kwani miundo mbinu ya maeneo ya Uzalishaji pia itaboreshwa katika utekelezaji wa mradi huo.

“Kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kuishukuru jumuiya ya umoja wa nchi za Ulaya kwa juhudi kubwa wanazochukua kusaidia maendeleo ya nchi yetu, asanteni sana,” alisema Waziri Dk.Mgimwa.

Naye balozi wa EU, Mhe. Filberto Sebrigondi alisema wameridhishwa na mikakati ya serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ndio maana wanaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kusaidia wananchi kufikia maendeleo ya kweli hivyo wameamua kusaidia sekta ya miwa ili iweze kukua na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

Pia balozi Sebrigondi alisema kuwa wataendelea kusaidia bajeti ya Serikali ya Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuwa Tanzania imeonyesha nia ya dhati katika kukuza uchumi wake na kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wake ili waongeze tija katika uzalishaji.

Alisema katika kipindi kilichopita asilimia 87% ya fedha lizizotolewa kwa Serikali ya Tanzania zimeshatumika katika miradi ya maendeleo, hivyo ameahidi kuwasaidia wanachi wanaojihusisha na kilimo cha miwa ili kuwajengea uwezo, kufanya tafiti na kutoa elimu ya utunzaji mazingira katika maeneo yatakayonufaika na msaada huo.

Umoja wa nchi za Jumuiya ya Ulaya umekuwa kwa muda mrefu ukisaidia sekta mbalimbali za maendeleo hapa nchini ikiwa ni moja ya washirika wa maendeleo wa Tanzania ambapo baadhi ya Sekta zinazonufaika ni sekta ya kilimo cha Kahawa, na Miwa, sekta ya Barabara, Elimu, nishati ya Umeme ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...