WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali ina kazi kubwa ya kushughulika na kundi dogo linalojihusisha na lugha za uchochezi wa kidini ambao unachangia kudhoofisha amani ya nchi.
 
“Tunajua nia yao ni kufanya nchi isitawalike lakini sisi tumesema hatukubali. Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, ulinzi uimarishwe kila mahali, mshingae kuona watu wanawahoji lakini nia njema, ya kurudisha amani yetu,” alisema Waziri Mkuu.
 
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Mei 10, 2013) wakati akiwasilisha salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya waumini watatu wa Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa mabomu uliotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, mwaka huu kanisani hapo.
 
Waziri Mkuu amewaomba wanachi kutoka ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kwenye upelelezi wa tukio hilo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2013

    tanzania tunajivunia amani ya muda mrefu sasa lakini kwa muda mrefu pia uvunjaji wa amani,mali na lugha za kukashifu dini za watu wengine imekuwa pia ndio utamaduni wa nchi hii na serikali ama kwa kujua au kufumbia macho imechangia haya majanga yanayojitokeza sasa.
    imekuwa jambo la kawaida kusikia maandamano ya waumini wa dini kupita na kutukana serikali au dini pinzani sasa matusi hayatoshi tumeanza kuona mauaji ya mapadri na mabomu makanisani.
    mimi napenda kuwaomba waumini wa dini zote kuwa wavumilivu na kuendeleza ustaarabu wao wa muda mrefu kwani ushenzi huu unaletwa na watu wachache wasioijua hata hiyo dini yao inawataka wawe watu wa aina gani,sasa wajinga wa aina hii namna ya kuwashughulikia ni moja tu kusiwe na "dialoque' za kipumbavu kwani nchi yetu ina uzoefu wa kuzifungulia tume matatizo wanayoyaogopa iwe muungano,wizi etc.
    hili la udini msilitafutie tume hayo mambo ya kikomunisti muachane nayo hili linataka utendaji wa kisheria,haki za binadamu na nguvu za dola kwisha.
    asante.
    mdau.
    mpakani na msumbiji.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2013

    NAFIKIRI TUFANYA APROACH YETU SCIENTIFICALLY. UNAVYOSEMA KUKASHIFU DINI NYINGINE MAANA YAKE NINI? NA UNASEMA ACCORDING TO WHAT? MFANO: WAHINDU WANAAMINI KWAMBA NG'OMBE NI MUNGU WAO. SASA ANAYESEMA NG'OMBE SI MUNGU KWA MUJIBU WA DINI YAKE ATAAMBIWA ANAKASHIFU DINI YA WAHINDU? NA AKIWA NA NAFASI HUYO MTU ATAKUWA ANAJARIBU KUMUELIMISHA HUYO ANAYESEMA KUWA NG'OMBE SI MUNGU KWA MUJIBU WA REJEA.

    KWA HIYO TUWE MAKINI; TUSIJE TUKAJIFANYA TUNATAFUTA SULUHISHO WAKATI NDIYO KWANZA TUNAZIDISHA MPASUKO. CHA MSINGI NI UVUMILIVE.

    ANAYESEMA NYOKA NI MUNGU WAKE AENDELEE KUABUDU. DINI MBALI MBALI WAZUNGUMZE UTOFAUTI WAO ILI WAUMINI WA DINI HIZO WAJUE HUO UTOFAUTI.

    KUNA VITABU VINGI VINAELEZEA HISTORY OF RELIGIONS. HII INAMSAIDIA MTU KUWA NA UFAHAMU NA KUWA NA UVUMILIVU NA NYINGINE KWANI ANAELEWA KILA DINI NINI KINAABUDU.

    UNGENIULIZA MIYE NINI KIFANYIKE: KUNGEANDALIWA HALLS/MAENEO KATIKA KILA MKOA/WILAYA AMBAKO KILA WIKI AU MWEZI KILA DINI ILIYOKO TANZANIA IENDE IKAELEZE DINI YAKE KWA WANANCHI. ILI WANANCHI WAWE NA UELEWA WA DINI MBALI MBALI. HII ITASAIDIA KUVUMILIANA. MTU ANAYEELEWA NI RAHISI KUVUMILIA KULIKO ASIE ELEWA.

    MUUMBA ATUSAIDIE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...