Home
Unlabelled
adha ya foleni jijini dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hahahahaha, hizi ahadi za barabara za juu na shida hii inayowasumbua sasa wakazi wa Dar naifananisha na ule ubeti wa mabomba ya maziwa nchi nzima au ahadi ya kuwapeleka mwezini wananchi wote.Hii kero haitaisha na itazidi kuongezeka iwapo viongozi watakua na ukiritimba wa kupeleka kila kitu Dar es salaam.Ipeni fursa mikoa mengine ili watu wajivute huko, kwani hata vyombo vya usafiri navyo pia vitajivuta huko na hatimae kumaliza msongamano.
ReplyDeleteKiswahil fasaha ni "ADHA" ikimaanisha Kero. Siyo HADHA, kama mlivyoandika kwenye hicho kichwa cha habari.
ReplyDeleteHK siku hizi hakuna waandishi wa Kiswahili sijui wanaandika kilugha cha wapi nimeshangaa hata BBC Swahili wanaandika utumbo lazima BAKITA iingilie kati ama kiwekwe chombo cha kusimamia print media maana mambo yanaenda bora liende na watu wanaonekana wameridhiiika na kukubali kinavyo haribika. Sasa ukiona na humu kwa Ankal kuna mchemsho sijui hao wengine tusemeje
ReplyDeleteNyie mnaolalamika hapo juu kuhusu utumizi bora lugha hamjachangia chochote cha maana zaidi ya kuangalia makosa ya maandishi.....Kinachojalisha ni kuwa MESSAGE IMEFIKA.... Mijitu mizima mnalalamika eti ni Adha sio Hadha. Nonsense. Changieni kuhusu ripoti mliyopewa sio makosa ya maandishi. Kama huna chakuongea kaa kimya...Anyways...foleni ni kero kubwa sana dar. Miundombinu haiendani na ongezeko la magari barabarani. Kinachotakiwa ni kujenga fly overs. Sio kitu kigumu kufanya hivyo kwani serikali itarudisha hela yake au kampuni binafsi kupitia mapato watakayopata kwenye tolls. Njia nyingine ni kuhamisha au kujenga ofisi mpya nnje ya jiji la dar es salaam. Kwanini kila mtu atake kuweka ofisi posta na sio bunju? Wekeni ofisi nnje ya mji au mpaka nije niwajengee mwenyewe?
ReplyDeleteHakuna kitu kibaya kama kujifanya mjuaji kwa kila jambo,kuna ubaya wa kusahihisha maneno kama mwandishi amekosea?ndo maana kuna mhariri kazi ndio hiyo na Ankal yupo ktk hii tasnia ya habari kwa miongo kadhaa sasa,hivyo tukimwona anaenda ndivyo sivyo lazima tumsahihishe.
Delete
ReplyDeleteTena siku hizi kuna msemo "lisaa" hakuna lisaa kwenye kiswahili ni saa au masaa kadhaa
Solution ya foleni za dar ni Main junction iziwe na by pass au tunnel.Hii nina maanisha nini ebu tutizame junction kubwa zote,yaani Tazara,magomeni ,fire,mwenge,vijana,uhasibu,kamata,karume,kigogo zinatakiwa hizo njia sizikutane lazima mmoja apite juu au chini hapo foleni haiwezi kuwepo na mzungoko wa magari utakuwa sio wa kusimama na kubadilisha njia zinazoingia kwenye mail road ziwe one way ili kupunguza foleni.Ukitoka gongo la mboto bila kusimama unachukua dakika kumi na tano umefika mjini lakini kila main junction lazima usimame foleni haito kwisha kwa kutegemea mataa yenu.
ReplyDeletenawakilisha
Msanga mkuu sailor.
SOLUTION, ni kwa serikali kutoruhusu ofisi au biashara yeyote mpya kufunguliwa mjini, na pia makampuni makubwa kama tanesco na mabenki yenye wafanyakazi wengi kuamisha ofisi zao kutoka mjini na kuzipeleka nje ya mji, na mwisho ni kuamisha makao makuu ya wizara zenye wafanyakazi wengi kutoka mjini kwenda nje ya mji
ReplyDeleteKama kweli mkataa kwao ni mtumwa, basi mimi nitafia utumwani. Hiyo adha ya nini, Kitwana? Ngoja nijibee boksi langu lakini bila pressure za kuingilia daladala madirishani. Huku jioni ukifika home hakuna umeme. Maji yanatoka bombani mara 1 kwa wiki 3!
ReplyDeleteWewe Anon. wa nne hapo juu, usilete ujuwaji wako, waache wenzio watowe maoni yao jinsi wapendavyo, hujuwi kila mtu ana uhuru wa kutowa maoni yake juu ya chochote kile anachokiona kimekosewa au kuhitaji marekebisho, alimradi kinahusiana na habari husika, iwe ni kichwa cha habari, picha au tukio chochote kile. Kuchangia unaweza ukachangia katika mtindo wowote ule, uwe wa kukosowa, kuelimisha, kuelezea na hata kwa kusaili. Makosa kama hayo madogo madogo yanaweza kuathiri na kupotosha maana nzima ya habari husika. Mbona wamerekebisha mara moja na kuandika inavyostahili ADHA, watuandikie HADHA kwani tunajifunza kiarbu.
ReplyDeleteFlyovers sio lazima, kitu muhimu kinachotakiwa ni ubunifu,nidhamu na adhabu. Ukitoka bunju unakwenda ubungo, kimara au kibaha na nje ya mji inabidi uje mpaka mwenge wakati inaweza kubuniwa barabara katikati ikapasua short cut na ikakatiza mpaka gongo la mboto na uwezekano kama huo upo sehemu nyingi tu. Vile vile barabara za mjini inaweza kupasuliwa barabara toka ilala mpaka kinondoni via upanga na moscow au gerezani railway mpaka keko, kurasini na temeke, na pia majority ya magari yaliyopo barabarani hayana hadhi ya kuwa barabarani. Pia kama maoni ya wengi pia kuhakikisha mtu anaweza kumaliza maswala yake popote kama tegeta, mbagala kimara au kinondoni sio lazima kila kitu kiwe kariakoo na posta lakini kama maoni yangu hapo juu tunahitaji ubunifu, nidhamu na adhabu. Ubunifu wa kuendeleza utendaji kazi bora, nidhamu ya kufanya kazi na uwajibikaji na adhabu kwa wanaovunja sheria, Sio polisi na watendaji wengine wa serikali kula wao pesa za adhabu na hakuna uwajibikaji na kuweka adhabu kali tu za barabarani ( e.g taa haiwaki laki 2 au 3) na toll ya kuingia mjini pia kupunguza ushuru kwa daladala. Miezi 18 akipewa mtu yeyote mwenye elimu ambaye si mwizi na mtendaji na akipata ushirikiano wa serikali kutakuwa na mabadiliko wazungu hawana akili zaidi ila ni watendaji na wana nidhamu tu tumesoma nao.
ReplyDelete