Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) aliyemwagiwa Tindikali na Mtu asiyejuilikanwa huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa pili kulia Kaka yake Sheha Sudu Mgeni Saidi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuangalia Sheha wa Shehia ya Tomondo Wilaya ya Magharibi Unguja,Mohamed Saidi Kidevu,(kulia) jinsi alivyoathirika na Tindikali alilomwagiwa na Mtu asiyejuilikanwa huko Tomondo juzi wakati alipokuwa akirudi kuchota maji na kuelekea nyumbani kwake,Sheha huyo yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja kwa matibabu,wa kushoto Dk.Slim Mohamed Mgeni,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Sijui kwanini jamani lakini watu wanafanya hivi, walau basi waseme wanataka nini ili ijulikane kuliko kuumiza watu.Kuweni wazi mnataka nini??
ReplyDeleteubinaadam haupo tena ila umebaki unyama. mimi nadhani kuwekwe sheria kali kwa wakosaji kama hawa sio kuwanyoa ndevu tu na baadae kuwapa dhamana. inatakiwa akipatikana basi na yeye amwagiwe tindikali.
ReplyDeletehahaaaa anony no 2 unasahau yesu amesema nini? ukipigwa kofi shavu upande mmoja basi mgeuzie na shavu la upande wa pili akupige , sasa hii tindikali kwa tindikali imetokea wapi?
ReplyDeletekwa hiyo aegeshe shavu lingine hilo amwagiwe tindikali ....
ReplyDelete