Nimesoma hoja hii kwenye blog moja kwamba Adam Nditi mchezaji wa Chelsea yuko tayari kucheza national team lakini hajawahi kuitwa na kuna baadhi ya wapenzi wanatoa lawama nzito kwa chama cha Mpira na viongozi wandamizi wa TFF. Mimi kama muumini wa soka la bongo naomba nitaharishe chama cha mpira ili tusifanye yale ya zamani ya kumleta Kally Ongala huku tukijua ana uraia wa Uingereza na huku Tanzania sheria zetu zikiwa haziruhusu mtu kuwa na uraia wa Nchi mbili (Dual citizenship).

Adam Nditi yuko Uingereza toka akiwa  mtoto mdogo kabisa hivyo sidhani kama kweli kijana huyu anaecheza Chelsea akawa anatumia passport ya Tanzania, ni na wasiwasi hatuna taarifa Za kutosha kuhusu huyu kijana. Ni kwasababu hiyo hatuwezi kukurupuka na kuwaandama viongozi wa TFF wakati hatujui status ya mchezaji mwenyewe.

Naomba kutoa hoja,

Onesmo Waziri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2013

    huyu mwingereza banaa tusidanganyane hapa..sema labda wazazi ni watanzania kwa kuzaliwa but nao pia ni waingereza kwa sasa...cezea passport nyekundu ww!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2013

    Mdau, nafikiri sheria za FIFA zinaruhusu mtu kuchezea nchi yake alikozaliwa hata kama ana urai wa nchi nyengine. Pia kama unaweza kuchezea nchi alikozaliwa babu au bibi yako. Kama Odemwingi, Moses, ambao wana uraia wa Russia na UK lakini wanachezea Nigeria. Tatizo la Wabongo walioko UK wengi wamejiripua Kisomali au Kirwanda ndio maana hawataki kujishughulisha na TZ maana itakuwa soo maana Mama mwenye siku hizi hana msamaha na wahamiaji haramu amewanunulia ndege maalum ya "Deportation".

    ReplyDelete
  3. MsemaKweliMay 29, 2013

    Huyu sio mtanzania. Ni Mwingireza mwenye asili ya Tanzania. Sasa atachezeaje Taifa Stars?

    Halafu hoja ya msingi ni kwamba hata kama anaweza chezea Taifa Stars hawezi fanya chochote yeye peke yake. Huu mchezo ni wa timu, kwa hiyo timu nzima inatakiwa iwe nzuri.
    Ni wakati wa kukuza vipaji vyetu wenyewe na si kukimbia vipaji vya watu walivyoviandaa.
    Hakuna programu ya kutoa vipaji, enzi zetu tulikuwa na umishumita, UMISETA hivi vitu hakuna tena. Tusitegemee maajabu mpaka kuwepo na prgramu inayoandaa vipaji.
    Huko Marekani kuna hii ligi wanaiita NBA, hivi wachezaji wake wanapatikanaje? Mbona mastaa huwa hawaishi? Kamaliza Jordan kaingia Kobe. Kobe naye anamalizia ngwe yake LeBron ndio kinara sasa. Tunaona vipaji vinaandaliwa tokea shule za sekondari, halafu wanaenda vyuo vikuu hakuna kata kona.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2013

    Umeuliza swali na kulijibu wewe mwenyewe!!

    Issue ya Adam Nditi ni sawa na ile ya kalimaganga Ongala. Umesema mwenyewe hudhani kama anatumia passport ya Tanzania ni issue ambayo hata Kali ilimtokea - je, Adam Nditi yupo tayari kuukana uraia wa Uingereza ili aje achezee Ngorongoro and/or Taifa Stars?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2013

    Drogba, na wenzie wengi wa Ivory Coast ni raia wa Europe sioni tabu yoyote

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2013


    Michuzi naomba ninukuu maneno ya Nditi kama alivyosema kwenye blogu ya Shafii Dauda,"Sijawahi kutafutwa wala kutumiwa mwaliko na TFF, ingawa siku zote nimekuwa tayari kwenda kuitumikia timu yangu ya Taifa kwa sababu mie bado ni mtanzania halisi kabisa."
    Kama wasiwasi ni uraia wake ubalozi wa Tanzania uliopo London ungetumiwa kufuatilia swala la kijana huyu. Iweje mwandishi wa habari atoke Tanzania ampate huyu kijana hapo London na ubalozi ushindwe?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2013

    Anonymous wa pili maneno yako kisu, hapa England wapo watoto wengi tu wa kitanzania ambao wanachezea West Ham, Crystal Palace, Leicester City na team nyingine na wengine wapo Scotland na kuna mmoja yuko even Scotland under 18 anaitwa Islam Feruz lakini tatizo ni wasomali na warwanda hata ikiruhusiwa dual nationality hawawezi kuja kuchezea national team ya TZ lakini wapo wengine ambao wazazi wao ni watanzania na wamewaleta huko kuchezea national team lakini viongozi wa TFF wakawakataa na nadhani Nditi ni mmoja wao kama kina Zidane walivyokataliwa na Algeria. Kuhusu uraia wa uingereza watu wengi wanadai wanao lakini si kweli maana mpaka kuupata ni shughuli kwelikweli wengi wana passport za UN za wakimbizi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2013

    WADAU NENDENI KWENYE GOOLGE MUANDIKE ADAM NDITI PLAYER PROFILE NI mtanzania amezaliwa zenji 1994 labda uniambie sheria za FIFA zinambana lakini kwa suala la uraia nop..unless uniambia alipofika 16yrs kachange uraia

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2013

    mtawala ni vigumu sana kusikiliza maoni ya wananchi anaowatawala ili kiongozi huwa anasikiliza maoni ya anaowaongoza, "viongozi" WENGI wa tanzania ni watawala, subirini siku wakiona kumfuatilia ndio njia bora ya kutawala, watamfuatilia. je watanzania, mmewahi kwenda ubalozi wa tanzania kuomba msaada? je hamkupewa moja ya majibu haya? KWA TATIZO LAKO HILI ITABIDI UFANYE MPANGO URUDI TANZANIA KWANZA UKASHUGHULIKIWE HUKO, au KWA HILI LABDA UMTAFUTE FULANI AKUSAIDIE UBALOZI HAUHUSIKI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2013

    Nimesoma sasa hivi kwenye Daily news soft copy, JAMANI MCHEZAJI HUYU KIJANA NDITI ANASEMA YUKO TAYARI KUCHEZEA TIMU YA TAIFA SATARS SABABU YEYE KAZALIWA TANZANIA
    LAKINI AMEKIRI WAZI KWAMBA HAJAWAHI KUITWA NA TFF
    TFF CHANGAMKENI MUKAMILISHE TARATIBU ZOTE ZINAZOTAKIWA ILI KUMUITA KWENYE KIKOSI TUNA MATCH MUHIMU MBELE YETU
    TUMIENI KILA KINACHOTAKIWA KWA HARAKA ILI AJIUNGE NA STARS HUKO EYHIOPIA
    NI USHAURI WANGU
    DAR ES SALAAM

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2013

    Angalia hii link toka Wikipedia inaonyesha bendera ya Tanzania

    http://en.wikipedia.org/wiki/Chelsea_F.C._Reserves_and_Academy

    jibu ni hilo

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2013

    huyu Adam ni Mtoto wa Eric Nditi kama mnamkumbuka zamani alikuwa akichezea Kikwajuni na Pia Small Simba huyu alikuwa ni jirani yangu pale Kisimama jongoo Zamani alipotoka Bara alikuwa na kina Robert Limo miaka ya 80 na kina Inno cent Haule

    Alienda UK kama mkimbizi wa mambo yale ya Zanzibar 95 lakini ukimbizi haumuhusu Mtoto wake kwa kuwa ameenda mtoto wake kama vile ni dependent wa Wazazi wake.

    Jengine kuna watoto wa kizanzibari pia wengi kama mdau amesema lakini utawakuta ni wasomali au hata wakiwa ni Wazanzibari as long as washaclaim asylum hawaruhusiwi kurudi huko hilo ndioo linorudisha mpira wa TZ nguvu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2013

    Kinachotakiwa ni kama Mdau wa Pili alivyosema FIFA inaruhusu Mchezaji kuchezea nchi alikozaliwa ama aliko na asili nako ili mradi mwenyewe akiri hilo.

    Kinachotakiwa yeye mwenyewe Adam Nditi aweke uwazi kuhusu Status yake ili watu waanzie huko Geneva-Uswisi FIFA kufuatilia ikiwezekana Brazil 2014 awemo Kikosini kwetu.

    Ukiijua Sheria Duniani kuna lilalo shindikana?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 29, 2013

    Hivi kwanini Watanzania wasiruhusiwe kuwa na uraia pacha(dual citizenship) kwani kuna shida gani? Au ni wivu tu ili sie tunaoishi huku mamtoni tusipate haki zetu Bongo?
    Inashangaza sana hata Kenya wameruhusu lakini TZ kila kitu mpaka kiwe na maslahi kwa wakubwa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 29, 2013

    Tanzania inatakiwa iharakishe Suala la Pasipoti mbili haraka sana.

    Sababu:

    1.Tunakosa faida kubwa sana za Kimaendeleo kutoka kwenye Diaspora Community (Wana Tanzania waliopo nje, ili hali hata kama wamebadili Uraia wangali wana asili ya Tanzania kama wana mapenzi na asili yao wanaruhusiwa kushiriki masuala yote ili mradi pawepo na Kanuni na vigezo).

    2.Tunakosa manufaa ya Kijamii na MIHCEZO kama hivyo mnavyoona mtu kama Nditi kukosa nafasi ya kucheza Stars hukumwenyewe akiwa rahdi kwa hilo.

    3.Tunawanyima Watanzania nchini na walio nje nafasi na fursa za kujitanua Kiuchumi na Kijamii kwa faida ya nchi na ustawi wa jamii na watu binafsi.

    4.Tunakosa idadi kubwa ya Wataalamu kutokana na Mashariti magumu ya kukataa Raia wasio wa Tanzania kutumika ktk Maofisi na Idara za Umma ambako mahitaji ni makubwa ktk FISCAL DEFICIT.

    5.Uchumi wetu unadumaa World Bank imetoa ripoti ya kuwa Madiaspora wameweza kutuma US$4 Billion kuja Afrika kwa mwaka 2012 pekee, pia kama wangekuwa na Uraia wa nchi mbili wangeweza kupunguziwa gharama za utumaji wakatuma zaidi ya hizo na kujenga uchumi wa nchi zao.

    6.Uhamishaji wa Tekinolojia unategemea sana Diaspora Community,(Technology Transfer) huku Uchumi wetu ukikua kwa kasi ya ajabu na ukihitaji kiu kubwa ya Maendeleo na uwezeshaji wa Kitekinolojia.

    7.Kwa kiwango cha mahitaji yetu kimaendeleo hadi KIUWEKLEZAJI tunakwama kuhamisha Mitaji,kufanya biashara kwa upana zaidi na kuwekeza kwa kigezo cha Kanuni za nchi POLICIES ambazo haziendani na mwendo au dira yetu, hasa suala hili la kujibana ktk kutotoa uraia wa nchi zaidi ya moja.

    Tunahitaji suala la URAIA WA NCHI MBILI LIHARAKISHWE ili kuleta faida nchini Tanzania.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 29, 2013

    Mtoa mada leo umegusa palepalee. Kwa kifupi ni kwamba huyu kijana anachezea Timu ya Under21 ya Scotland, inamaana uraia wa Tanzania hapo, Nehiii!!Lakini sio yeye tu yupo Mtoto wa Doctor Ngoma, anachezea Manchester City reserve team, mwaka jana alipelekwa Loan Barnsley FC. Crip zake zipo tu nyingi Youtube na kwingineko. Kuna mtoto anaitwa Madundo, yupo Coventry, nae ana mambo makubwa tu.
    Kingine Serikali yetu inashindwa kutoa maamuzi ya Uraia Pacha, ndio sababu ya yote haya. Watu wanaangalia maisha yao kwanza na familia zao, kabla kucheza Nationa Team.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 29, 2013

    mzanzibari huyu sio mtanzania, nyie wabara vipi?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 29, 2013

    Watanzania penye nia pana njia Prince Boateng kazaliwa Ujerumani lakini kachezea Ghana. Kama ni kweli tunawachezaji wa TZ daraja la kwanza huko Ulaya wananchi tupige kelele warejeshwe Taifa Stars. Dream yangu ni kuiona Taifa Stars ikicheza World Cup. Kama ni kuchukua njia za mkato hizo njia zichukuliwe jamani

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 29, 2013

    mimi nawaza tofauti...wacheza tunao wakutosha mchangani tuwe wazalendo wa kweli tuwatowe mchangani wapate kuliwakilisha taifa lao na hatimae kutoka...huyo ameshatoka tuwatowe wengine
    nawasilisha

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 29, 2013

    Sterling wa Liverpool ,yule dogo wa United Ghana ilimtaka England wakampa cap chap chap, dogo mwingine katoka Crystal Palace kwenda United hawana tofauti yoyote na Nditi. Kalou ni raia wa Holland, Drogba France
    Kitambulisho kuwakilisha Taifa ni Passport. Forget about dual nationality maana UK hawajali hiyo.
    Tumeona Wakenya wakikimbia Qatar, miaka ya nyuma wa Tz wamachezea soka Oman(as Omanis) na mkataba umeisha wamerudi bongo

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 30, 2013

    Mimi nadhani tatizo lipo maana kama alienda Uk ni mdogo hatujui hao wazee wake walikuwa wanaishi kama nani hapo uk si mnajuwa maisha ya Ulaya tena

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 30, 2013

    Wengi wameandika maoni bila elimu ya ADAM. Adam ni muengereza ana Passport ya UK. Ndani ya passport yake anatakiwa awe na Muhuri wa DUAL CITIZEN mtoto ambaye amezaliwa nje ya nchi au ana umri wa miaka chini ya 18 anakuwa anagongewa kwenye passport yake ikiwa Baba ake ana Passport ya Tanzania na amemuombea. Adam hana huu muhuri na akitimiza miaka 18 hii Dual anakuwa hato qualify tena. Hili sielewi kama Baba ake anayo Passport ya TZ bado kwasababu alikuja mkimbizi wa Zanzibar uk 95 huko, Kama anayo basi pia anayo ya UK kwa sheria za TZ ni makosa kuwa na uraia miwili. Adam ni Muengereza mpaka Tanzania mutapobadilisha sheria za uhamiaji na yeye mwenyewe kama ataamua kuchezea TZ inawezekana lakini kwa sasa Endeleeni kuota. Muacheni akuze kipaji chake Wa TZ TUENDLEE na choyo.. KUNA wamejifanya wasomali warundi waacheni watoto wacheni kuwapakazia kwenye masocial media na kutaja majina yao ujinga na choyo hicho.. ujanja kuwahi. Bila shaka wengi wapo waswahili muliyataka wenyewe Serekali ya Muungano ilikuja UK ikawapakazia wa Zanzibari waliokuja ukimbizi saivi TZ ingelikuwa inakula faida. Kuna watoto 70 mpaka 100 ambao wapo kwenye soka ya Uk wana kuzwa na naamini wapo wengi watao make kwenye level ya juu. Watoto wengi wa Kizanzibari football ni Nature. Yupo Adi Yussuf mbona Tanzinia hamunfuatilii.. anachezea Burton Albion ni Mzanzibari halisi wa kuzaliwa. http://www.burtonalbionfc.co.uk/team/player-profile/index.aspx?playerid=460536&tcmuri=154533 Mtazameni mtoto uyo, Mwambieni Rais aje kumfata.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 30, 2013

    Nadhani kuma mtu hapa ameongea kitu cha ukweli kama wazee wake walikuja kama wakimbizi ni pamoja na yeye alikuwa mkimbizi lkn haina maana hata kama unaPPT ya UK anaweza kuchezea Team ya Tanzania lkn pengine sababu katokea Znz ndioo maana hawataki kumuita kwenye hiyo Team,na kama mwenyewe yupo tayari kwa nini hawamuiti ina maana TFF ndio tatizo

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 30, 2013

    ADAM NDITI SIO MWINGELEZA WALA MZANZIBAR NI MNGONI WA RUVUMA ALIYEZALIWA ZANZIBAR NA BABA YAKE KWENDA UINGELEZA KWA HIYO ANAWEZA KUICHEZEA KILIMANJARO STARS AU AKITAKA TAIFA STARS

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 30, 2013

    Wabongo kwa jelous, nyie bishaneni wenzenu wanalipwa 20-30k weekly ! kuweni positive jamani hata once...........

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 29, 2014

    Ni kwelii watanzania wacheni watoto msiwatie midomoni wai peke yao hawatoifanya taifa kwenda juu lol acheni choyo..kila mtu kapangia risk yake na mwenyewe muumba

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 29, 2014

    Mh wabongoo lini mtabadilika kwa roho mbaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...