Kuna mambo kusimamiwa kwake kidete ni kukaa chini, mengine ni kulala na mengine ni kusimama wima. Kukiwa na jambo au hali haulidhiki nayo, machaguo yako mengi kuonyesha hisia na hata msimamo wako. Yote haya lazima yafanyike maadamu tu ujumbe ufike kwa ufasaha mahala husika wakati hatua sahihi zikiendelea na utekelezwaji. Haiwezekani kwenye nchi yenye tatizo la ajira linaloongezeka kila uchao vijana wenye vipaji wafe na njaa kisa tu ugomvi na madalali wa sanaa! 
Wasanii wanapaswa kufa na njaa pale tu kama kazi zao hazikubaliki na hadhira na hivyo hazinunuliki. Lakini suala la kufichwa na kufunikwa kwa jitahada za nguvu ya uwezo wa kifedha, mali na mtandao mpana ni la kupingwa kwa nguvu zote na hadhira. Lazima hadhira iwe ndiyo hakimu pekee wa kazi, maslahi na mafanikio ya wasanii. Haiwezekani hadhira ionekane ni ya muhimu tu katika kauli mbiu za kuteka masoko kibiashara lakini linapokuja suala la mahitaji, hadhira ichaguliwe na fanani nini inastahili kusikia, kuona, au kula. Hili kamwe haliwezi kuwa chaguo langu wala la hadhira au Watu. 
Ni chaguo la fanani na la stahili kusikilizwa, kuonwa au kuliwa na huyo huyo fanani na mafanani wenzake. Dhihaka inakuwa kubwa zaidi pale jambazi linapoongoza jitihada ya kutokomeza kazi za vibaka! Kweli mwenye nacho hujitwalia zaidi na sheria ni kipofu kwa mwenye nacho. Pamoja na yote haya, umma unayo silaha nzito na mahsusi yenye uwezo wa kuwaangamiza majambazi na kuwatokomeza vibaka. Silaha yetu ni umoja katika kupinga ufedhuri wa mafanani uchwara na dhihaka ya majambazi. Anayejitenga na umoja huu, anajindalia upweke msibani zamu yake ikifika. 
Ni masikitiko kwamba wanaodhurumiwa na kuibiwa wameanguka katika tego la kale la majambazi na wadhurumaji. Wametegwa wajitenge na umoja na wao kwa kujua ama kwa kutokujua wakategeka! Wamekubali kuutumikia mkate wa siku wa kafiri wasijue kwamba kesho safari ya dhuluma yaendelea! Na hawa watadumu katika safari ya kudhulumiwa milele na hawachomoki ng’o! Tunaochukizwa na yote yaliyosimuliwa hapo juu, tuungane na waliokwisha jitambua katika kujinasua na ufedhuri wa madalali uchwara wa sanaa. 
Tuwasaidie kupaza sauti za umoja katika kuwashambulia majambazi. Tuwaonyeshe mafanani uchwara na majambazi kwamba nguvu haziko kwao bali kwetu (hadhira). Tulidhirishe kwamba sisi ndiyo tunapaswa kuchagua tukipendacho maana twalipia muda, huduma na bidhaa. 
Tukatae kuchagulia nini kisikilizwe na masikio yetu, macho yetu yaone nini au vinywa vile nini na kisha watupigie kauli mbiu za “Chaguo la Watu” Ijumaa ya Tarehe 31 mwezi huu, tuliowengi hatuendi na kipaumbele cha kucheza disco, kuangalia wacheza disco au kusikiliza music live bali tunakwenda kusema hapana: “Unyonyaji haukubaliki na Kufanyiwa machaguo hakukubaliki”. Tutafanya hivyo kwa sauti kubwa na ya umoja. Tunakwenda kuthibitisha kuwa ni Sisi ndiyo hadhira na siyo wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2013

    Ujumbe murua, tupo pamoja.Laiti kama ningekua Tz nami ningeshiriki.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2013

    haya dada jide mwenzenu mangwea ndio hivyo kashatangulia mbele ya haki...kama kweli una-fight huo umoja utaahirisha hiyo event yako kwa heshima ya huyu nguli mwenzenu kwenye fani ya bongo flava?..au ndio umoja kwenye maslahi binafsi tu?..mtihani mzito huu..!!!

    j4
    ujerumani

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2013

    huo ugomvi wenu utakwisha lini? mnatuchosha na ngonjera zenu,...we jide kwa nini usifanye kazi zako tu badala ya kuendelea kutunishiana misuli ya watu wengine??? watanzania hatupendi magomvi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2013

    Uncle, Jide anahitaji psychological treatment na pia sasa hivi c mtu wa kumuamini sana kwa anachotetea, yeye anapigania maslahi yake tuu na sio wasanii wadogo na hii yote ni kutokana na ushindani alioupata kwenye band yake, sasa uncle ni bora kukaa pemben kwa ugomvi ambao hujui mwisho wake utakuja aibika uncle......

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2013

    Mwanzo mzuri

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2013

    Dada yetu Jeydee funguka sawasawa. Kiasi fulani nimekuelewa lakini specifically tungepata kujua hawa majambazi na mafanani uchwara ili tuungane pamoja kuwapinga vikali. Nimeipata ya 'chaguo la watu' lakini wengine sijawajua.
    Halikadhalika sjjakupata vizuri hawa 'chaguo la watu' nini tatizo lao ktk tasnia maana kwa mtazamo wa sisi hadhira tunaona kama hawa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuwapromote wasanii hapa nchini hasa wa muziki wa kizazi kipya.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2013

    Maneno mengi sana yanachosha kusoma, yangeweza kuandikwa kwa mistari miwili tu na ujumbe huo huo ukafika. Nimepata shida sana kutafuta ujumbe ktk maneno mengi namna hii!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2013

    JIDE DADA YANGU, SASA HIVI KUNA CHALLENGE SANA KATIKA BONGO FLAVOR, LAIMZ UKUBALI MABADILIKO DADA USIPANIC KILA MTU ANATAKA KUWA KAMA WEWE, NA VIJANA SASA WANAFANYA KAZI KWA NGUVU, WEWE HUPIGANII MASLAHI YA WOTE NI YAKO PEKE YAKO BANA(reference J4 ujerumani)..

    jaribu kutafuta mbinu mpya za biashara, unaongea sana kama taarabu.. kwani mwanzo mbona ulikua unashirikiana nao vizuri??ulikua hujui kama wezi??..hapa ni kuzidiwa tu kibiashra dada, jipange acha maneno, watanzania tunapenda kurushiana sana maneno badala ya kuangalia na kupanga strategies mpya na kuosonga mbele.

    sio wewe tu, hata sisi wafanya biashara kuna kipindi hali huwa zinkua tete sana, ila tunajipanga na kusonga mbele, wewe si unasikia makontena yetu sasa??hili ni balaa na ni hasara.

    ACHA MANENO YA TAARABU, FANYA KAZI NA ANGALIA CHANGAMOTO, BAND NI NYINGI SANA KWA HIO UKIISHIA KUTAFUTA SYMPATHIES KWA WATU, UTAKUA KAMA SISTER P NA ZAY B.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2013

    Where is machozi band?It doesnt feature anywhere in adverts.It is the Lady only,seems alone!But the whole is stronger than sum of its parts.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2013

    Tupo Pamoja JD. Usingeahisirhsa show bali ungedonate part ya proceeds kwenda kuchangia kuleta mwil wa Ngwair.

    Hawa wanaoita huu ni ushindani wa biashara hawajui ushindani una mipaka na kuna vitu havuiruhusiwi kumtendea mshindani wako. Hiyo ipo duniani kote. Inahusu Monopoly Power kutotakiwa. Waangalie sheria za huko wanakopenda ughaibuni. Kampuni hairuhusiwi kumili msanii,kumili vituo vya TV/Redio kumrusha msanii wao, hairuhusu kuandaa matamasha kwa kampuni hiyo hiyo, hairuhusu kuhonga madj (payola)na watu huenda jela kwa hilo, hairuhusu kuhonga 10% kwa Marketing Mgrs wa Voda/TBL/Serengeti etc waipe kampuni hiyo hiyo tu hela za matamasha wengine mnaambiwa mpitie huko kwa hao kama una tamasha na mengi mengi tu...

    tatizo tanzania ndio maana utandawazi na fursa ya biashara tuliohubiriwa imetufanya kuwa maskini ! BIASHARA ZINA SHERIA NA USHINDANI UPO ULIO HALALI NA USIO HALALI, SISI TUNADHANI KUSHINDA BIASHARA ZOTE NI SAWA NA KUSHIND KUNA-JUSTIFY MEANS. Ni kutoelewa kunatuponza. Tufunguke.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2013

    Hahahahaha !!!!!

    Tafadhali tujuzane,

    Mdau wa 8 umenikumbusha mbali saaana hivi wakali wetu wa longi Sister P na mshindani wake Zay B wapo wapi?

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 30, 2013

    Jide Dada yetu Mpendwa Ze Komandozzz ukisika KULA KWA TINDO ndio hukooo!

    Hapo ndio unatakiwa uutumie U Chuck Norris wako na Ukomandoo wako kukabiliana na Msala na Changamoto hizo za upinzani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...