Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally Isere (kulia) akimkabidhi jezi seti moja Dige Shaaban Nkusa kwa ajili ya timu ya vijana wa kijiji cha Mwembeni wilayani Kondoa ili kuimarisha michezo vijijini.

 KAMPUNI ya Isere Sports imetoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 1.7 kwa ajili ya kuendeleza vijana katika wilaya ya Kondoa.

Akikabidhi vifaa hivyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Sports, Abbas Isere alisema ametoa vifaa hivyo ili kuwasaidia vijana kupenda michezo ili kujenga afya na kujikinga na vitendo vya uhalifu. 

Abbas alisema vifaa alivyotoa ni kwa ajili ya vijiji vya Changaa kwa Mafunchi ambako wamepewa jezi, mipira na soksi, katika kijiji cha Mwembeni kata ya Hondomairo wilayani Kondoa wamekabidhiwa vifaa kama hivyo.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya vijana wa Changaa, Issa Lubuva alisema umefika wakati kwa wananchi waishio mijini kuwakumbuka vijana waliobaki nyumbani kwa kuwapatia vifaa vya michezo.

Naye Dige Shaaban aliyepokea vifaa kwa niaba ya kijiji cha Mwembeni alisema wachezaji wengi wapo vijijini lakini hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao hivyo vifaa hivyo vitasaidia kutoa wachezaji kutoka wilaya ya Kondoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...