Na Abdulaziz Video,Lindi
Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za
kusambaza taarifa za kupotosha wananchi zenye viashiria vya uchochezi
na vitisho kwa serikali kwa lengo la kuvuruga amani, upendo na utulivu
wa wananchi.
Akitoa taarifa kwa wandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Lindi George Mwakajinga amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na
mabango yenye maandishi ya uchochezi kwa watu wa mikoa ya Kusini.
Amesema kati ya watuhumiwa hao wawili, mmoja anatambuliwa kwa jina la
Ivon Vandu Taasa mkazi wa Sabasaba ktk Manispaa ya Lindi ambaye
alikutwa eneo la kituo cha mabasi ktk Manispaa hiyo akihamasisha
wananchi kuunga mkono vurugu zinazofanywa na wananchi wa Mkoa wa
Mtwara akiwa akiwa na mabango ya karatasi yenye maneno "Gesi kwanza
Uhai baadaye".
Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi, mtuhumiwa mwingine ambaye jina
lake linahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi, anatuhumiwa kusambaza
ujumbe wa simu kwa watu mbali mbali zenye kuchochea na kutoa vitisho
dhidi ya serikali na jamii na katika tukio lingine Mkazi wa kijiji cha
Majengo wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Silvanus Patrick,
anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa
kidato cha pili ktk shule ya sekondari Msufini wilayani humo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi George Mwakajinga amesema kuwa
mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo usiku wakati mwanafunzi huyo
akitokea dukani alikotumwa na wazazi wake kununua mafuta ya taa kwa
matumizi ya nyumbani kwao.
Mwakajinga amesema baada ya mwanafunzi huyo kudai kufanyiwa kitendo
hicho, aliwaarifu wazazi wake ambao walitoa taarifa kituo cha Polisi
wilaya ya Nachingwea na kufanikiwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Mwakajinga amesema kutokana na kitendo hicho, mwanafunzi huyo
alipelekwa hospitali ya wilaya ya Nachingwea kwa uchunguzi wa
kitaalamu na kubainika kufanyiwa kitendo hicho na kwamba mtuhumiwa
anatazamiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya polisi kukamilisha
taratibu zote za kisheria.
Kwa sasa mbona wachochezi ni wengi tu. Ishakua kauli mbiu.
ReplyDelete