Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Steve Gannon akionesha kizibo cha bia aina ya Serengeti Premium Lager chenye malekezo namna ya kujishindai zawadi mbalimbali,mbele ya wanahabari na baadhi ya washindi wa bahati nasibu waliowahi kujinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya bia hiyo.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu wakiwa sambamba na mmoja washindi aitwaye Rahma,aliyewahi kujishindia piki piki kupitia promosheni za kinywaji hicho cha Serengeti Premium Lager.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Steve Gannon akionesha namna ya kutuma ujume wa promosheni ya WINDA NA USHINDE kwa kutuma ujumbe kupitia namba iliyowekwa maalum kwa promosheni hiyo,mbele ya wanahabari na baadhi ya washindi wa bahati nasibu waliowahi kujinyakulia zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya bia hiyo.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu wakiwa sambamba na mmoja washindi aitwaye Rahma,aliyewahi kujishindia piki piki kupitia promosheni za kinywaji hicho cha Serengeti Premium Lager.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu “Kampeni na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja wetu,Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi. Bia hii inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi, tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya wateja wetu kujisikia kwamba wanadhaminiwa kwa njia moja au nyingine.,”alisemaBw. Mafuru.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Ephraim Mafulu akifafanua zaidi kuhusiana na promosheni hiyo ya WINDA NA USHINDE iliyozinduliwa leo ndani ya kiwanda cha kampuni hiyo,Temeke jijini Dar na kuhudhuriwa na Mkurugenzi mkuu (Group Managing Director) Bw.Charles Ireland na Mkurugenzi mkuu wa Masoko na Ubunifu (Group marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah.Shoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Bwa.Steve Gannon.
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzindu wa promosheni hiyo mapema leo,wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa SBL,Bwa.Steve Gannon alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu promosheni hiyo pia na pia kuwashukuru wateja wao wote ambao wamekuwa na wanaendelea kuwa nao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...