Kampuni ya Jambo Concepts (T) Limited,sasa imeingia kwenye biashara ya kisasa zaidi ya matangazo kwa kuweka electronic billboard kwenye viwanja vya ndege Tanzania.

Kwa kuanzia imeanza na kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere kwa kuweka LCD screen kubwa ya 9 X 3 na inapeleka kwenye viwanja vya ndege vya KIA na Mwanza.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo,Juma Mabakila alisema lengo kubwa ya kuweka LCD Screen kuba kwa viwanja vya ndege vya Tanzania ni kuondokana na viwanja vyetu kuweka matangazo ya kisasa ili kwenda na wakati na hususani kuweka matangazo sehemu yote ili kuondokana na utaratibu wa sasa ambao unaonekana kama hauna mpangilio. 

mbali na kuweka Screen hizo viwanja vya ndege pia itaanza kuweka katikati ya miji mikubwa ya Tanzania, kwani mbali ya kuweka matangazo lakini itakuwa kivutio na kupendezesha miji, tayari kwa kuanzia ipo mbioni kuanza na Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Juma Pinto (wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa masoko,Mabakila na mafundi waliotoka Dubai kufunga Csreen hizo uwanja wa ndege wa JNIA juzi tayari kwa kuanzia kazi.Screen hiyo kubwa imekuwa kivutio kikubwa airport hususan kwa abiria wanaoshuka kutoka nje ya nchi "International arrival'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2013

    me nadhani ilipofikia uwanja wa julius nyerere hauna hadhi hata ya kuitwa local(regional) airport let alone international airport.

    Kwa waliopita pale watakubaliana nami kwa jinsi mambo yalivyo ovyo ovyo kuanzia majengo,huduma&wafanyakazi...huu uwanja una hadhi labda ya kimkoa au kiwilaya.

    mdau
    uswisi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2013

    Acha ujinga wako wewe ushaenda airports za kimkoa ulaya na marekani hukuti hata mtu wakati mwingine. Kwa kuwa mmekaa ulaya ndio mnaiponda JNIA. Wengi wengi wenu wakuja mkiona choo cha kizungu mnakipandia juu badala ya kukaa na kwa sababu wengi mnapanda na viatu kinakua kichafu kila wakati kama unajua kiswahili basi utaelewa ninachosema. MWENDA TEZI NA OMO HUREJEA NGAMANI. Kwenu umejenga ghorofa unayokaa ulaya. Maana ukirudi kijijini utakaaje katika boma kama mmasai.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2013

    uwanja choka mbaya

    kuna sehemu zinavuja
    joto kali unatoka majasho ukiwa ndani
    huduma mbovu inanuka rushwa

    tanzania bado sana ankali endelea kutuonyesha vikwangua anga vya kina masawe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2013

    uwanja kwa kweli umechoka sana. Mdau wa kwanza yupo sahihi yaani huu unafaa kuwa uwanja wa wilaya sijui hata kama unafaa kuitwa uwanja wa mkoa. Huu sio international airport hata kidogo basi tuu hatuna kiwanja kingine na huu ndio nafuu nchi nzima kwa hiyo utaendelea kuitwa international. Jambo la aibu zaidi ni kuwa Serikali imefumbua macho na imeridhika na huu uwanja kwa hiyo hakuna kinachofanyika kuuendeleza au kujenga kiwanja cha maana. Tunakosa mapato mengi sana kwa ajili mashirika mengine ya ndege yamekataa kuendelea kuutumia huu uwanja, mfano ni British Airways haiji tena bongo.

    ReplyDelete
  5. Good Job Jambo, Hawa ni vijana wa kitanzania wanaoleta maendeleo kwa wenzao vijana, hii ni hatua kubwa sana. Kampuni hii inakua siku hadi siku rappidly

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...