Home
Unlabelled
KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU TAARIFA YA AWALI YA TUME YA TAIFA YA KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
KUHUSU ELIMU TAALUMA ITUMIKE HASA NA SI SIASA. NINACHOOMBA ELIMU IFUNDISHWE KWA KISWAHILI. IVI MTU AKIFUNDISHWA JINSI YA KUTENGENEZA MELI YA KIVITA SI NDIYO ELIMU YENYEWE??? AU ELIMU NI KUZUNGUMZA KIMOMBO??? MIYE NINACHOJUA NI KWAMBA UNATAKIWA UJUE KUTENDA JAMBO HALAFU UTAFUTE NJIA BORA YA KUWASILIANA. MTANZANIA ANAZUNGUMZA KISWAHILI KILA KONA NA KILA WAKATI; UNAMLAZIMISHA KUTUMIA KIINGEREZA SHULENI UNAMPA TABU TU. UTAONA UNAINGIA FORM ONE UNAFUNDISHWA WHAT IS CHEMISTRY? AU WHAT IS BIOLOGY? AU WHAT IS PHYSICS? N.K. WAKATI SHULE YA MSINGI AMEJIFUNZA MAANA YA FIZIKIA, ELIMU YA VIUMBE, N.K. MIYE KILA SIKU NASEMAGA; NCHI YETU BADO UKOLONI UPO; WE ANGALIA TU HATA BENDERA YETU INAPEPEA NUSU SIKU; SASA SIJUI ILIVYOPANDISHWA SAA SITA ZA USIKU MWAKA 1961 ILISHUSHWA SEKUNDE KADHAA BAADA YA KUPANDISHWA HAFU ASUBUHI IKAPANDISHWA TENA??? KAMA HATUJAIINGIZA MAANA YA BENDERA KUPEPEA MASAA YOTE KATIKA MIILI YETU BADO HATUJA ELEWA UHURU NI NINI??? HAYA WATANZANIA WENZANGU TUCHAPE KAZI; NDIYO KIZAZI CHENYEWE HICHI TUWAACHIE WANAOKUJA TANZANIA YENYE KHERI. MUUMBA AIBARIKI TANZANIA NA AJAALIWE VIONGOZI WETU WAFANYE UADILIFU KWA RAIA ZAKE NA UWALINDE NA KILA LILILO NA SHARI.
ReplyDelete
ReplyDeleteMatokeo yafutwe, inashangaza!!! Hao wanafunzi wapo ready kurudia? Na wapo wapi muda huu? Na pia nani anaingia gharama za kurudia mihithani? Na majibu yakiwa mabaya je? Kwa nini wasistandardize bila kurudia?
Kiswahili ni local language sio academic na haifai kutumika kwenye academic.
ReplyDeleteUngejua ni Watanzania wangapi wanakosa kazi kwa kutojua Kiingereza usingeandika hayo maneno.
Kiswahili utapeleka wapi? Kilikuwepo Kilatini na Kigiriki vikafa sembuse kiswahili?
Ni wakati sasa elimu kuanzia chekechekea itumie Kiingereza.
Ukitaka wanao waje kuwa omba omba, wakataze wasijifunze Kiingereza
Kiingereza kifundishwe kama somo la lugha.Ila masomo yanayotaka ufikiriaji wa ndani kiswahili kitumike ili kuzalisha wataalamu wa kweli na sio wa kubabaisha na walionakili kama ilivyo sasa.Kuna nchi nyingi duniani wameendelea sana na wanatumia lugha zao kama ujerumani,uchina,uswede,wafinn,wanorway,wafaransa,wajapani n.k.Andikeni vitabu vya kiakademiki kwa kiswahili kama vitabu vya kufundishia na maendelea yatakuja.Kinachotakiwa ni maarifa na sio kujua kiingereza tu.
ReplyDeleteMtoto wa Kabwela.
Sweden
Anonymous wa May 03, 2013 bado hujajua maana ya elimu. Huwezi kusema kwamba kiswahili ni local language kwa hiyo haiwezi kutumika kwa ajili ya kujifunza jinsi ya kufanya "MATHEMATICAL MODELING" YA "ANY COMPLEX SYSTEM", huwezi kutumia kiswahili kufanya "DESIGN YA DRONES"; huo unaitwa ni UKOLONI;yani kufikiria ni hasa elimu maana yake. Najua hii imetokana na ukoloni tulioletewa na unaendelea kututafuna. Wachina kule kwao wanatumia Kichina nayo ni local language; wajapani wanatumia kijapani nayo ni local language n.k.
ReplyDeleteKinachotakiwa kufanyika ni kwamba lugha kama lugha mtu ajifunze ili kuongeza mawasiliano na watu mbali mbali. Lakini maarifa ya kujifunza kuleta maendeleo ya Tanzania yatolewe kwa lugha inayoeleweka ambayo ni kiswahili ambacho kinazungumzwa na kila Mtanzania na sasa nchi zaidi ya 13 zinazungumza.
Najua ndugu yangu hapo umeathirika na ukoloni; pole sana. Maana wako wengi kama wewe wanaofikiri kwamba bila kiingereza nchi haiwezi kuendelea. Kwa taarifa yako mafundi welding waliojifunza mtaani ndiyo wanaotumika sana katika kazi za "JOINGING". Sasa huyu wa welding anatakiwa aongezewe ujuzi na yule anayejua kwa kumueleza tu kwamba ukitaka kuunganisha aina hii ya ghafi aina nzuri za "ELECTRODE" ni hii; kwa kuwa zinashabihiana. Hiyo ndiyo elimu na unaelezea kisayansi kwa nini kinafanyika ivo.
Utakuta mahakamani pia hukumu inasomwa kwa kiingereza; mtuhumiwa kiingereza hajui. Sasa sijui unamsomea nani??? Ukisikia Taifa halielimika ni ivo. Kwa ujumla tunakosa DETERMINATION.
Na nakueleza kwa uhakika kwamba Kiswahili kisipotumiwa kwa taaluma yetu na makabrasha yote yanayohusu taifa la Tanzania maendeleo yatachukua miaka mingi. Sababu kubwa ni mawasiliano kati ya Watanzania na kinachotakiwa kielimishwe ni mdogo sana.
Anyway ni changamoto zenyewe; kazi njema.
WEWE ENDELEA KUKARIRI KWAMBA KISWAHILI NI LOCAL LANGUAGE; UNASAHAU KWAMBA KONGO, KENYA, UGANDA, MSUMBUJI, N.K. WANAZUNGUMZA KISWAHILI.
ReplyDeleteNGOJA NIKUULIZE WEWE NDUGU WA HAPO JUU; UNAVYOSEMA SIYO ACADEMIC UNAMAANISHA NINI?
KWANI MTU AKITAKA KUJUA KUBADILI "GENES" ZA MCHICHA ANAHITAJIKA AJIFUNZE NINI??? NA JEE KAMA MAELEZO YA JINSI YA KUBAILI "GENES" YA HUO MCHICHA YA KAANDIKWA KWA KISWAHILI NA YULE ANAYEJUA KUFANYA HIVYO HAITAKUWA KWAMBA ANAYEJIFUNZA TAALUMA HIYO TAYARI AMESHAFANYA WAJIBU WAKE NA MTANZANIA ANAKUWA AMEPATA TAALUMA KWA WELEDI ZAIDI???
SASA NDUGU TAALUMA SI NDIYO HIYO.
AU UNATAKA MZUNGU AJE AZUNGUMZE KUHUSU GENES MODIFICATION KWA KIINGEREZA HALAFU AKITOKA MUPIGE MAKOFI NA KUSEMA JAMAA ANZUNGUMZA KIMOMBO VIZURI SANA. UKIULIZA UMEJIFUNZA, UNASEMA INABIDI NIKAANGALIE KWENYE KAMUSI??? HAPO TUTAFIKA???
NCHI HAIWEZI ENDA KWA MTINDO HUO.NDIYO MAANA MIKATABA MINGI NI MIBOVU; ANAYEPEWA KWENDA KUSIMAMIA ANAKUWA HAJUI KILICHOANDIKWA NUKTA HADI NUKTA. ANAPIGA SAHIHI TU BASI; ILI ASIONEKANE HAJUI KINGEREZA. ANASAHAU MADHARA YATAKAYOPATIKANA KWA TAIFA LAKE.
MUUMBA UTUJAALIE TUWE WENYE KUELEWA NA UIJAALIE NCHI YAKO YA TANZANIA IWE NA WATU WENYE KUELEWA MAANA HALISI YA ELIMU.
Wewe jamaa wa tatu unahitaji kuelimishwa. Tunao watanzania wengi wanaenda nchi mbali mbali kujifunza ujuzi. Mtanzania anayeenda ujerumani anajifunza kijerumani halafu anaanza masomo yake mfano ya utabibu. Akija tanzania anaendelea na kazi; lakini ukiangalia hicho kijerumani hakitumii sana na kama anakitumia ni yeye kama yeye.
ReplyDeleteIvo ivo kwa anayeenda kusoma nchi zingine kama china,sweden,denmark,korea ya kusini,japani,n.k.
Watanzania wanajifunza kiswahili wanapotoka tu tumboni kwa mama. kwa hiyo tunategemea ataelewa vizuri zaidi taaluma atakayofundishwa kama lugha ya kufundisha ni kiswahili.
Fanya jaribio moja. uandae mada kwa lugha mbili tofauti. mfano mada ya kufuga kuku wa kienyeji. uandike kwa kiingereza halafu ukamfundishe mtanzania. ifanyike kwa muda wa wiki mmoja. na mada hiyo hiyo uiandike kwa kiswahili halafu umfundishe mtanzania kwa muda wa wiki moja.
Halafu wafanyie mtihani ili uone nani atafanya vizuri kati ya makundi hayo mawili. Jawabu utakalopata utajua ni lugha ipi ni sahihi kutumika katika elimu
Kwa kukusaidia tafuta ripoti tafiti zinazohusu lugha sahihi ya kujifunza. Hapa Tanzania majaribio yalishafanyika na ikagundulika kwamba wanaofundishwa kwa Kiswahili wanafanya vyema maradufu kuliko wanaofundishwa kwa Kiingereza. Tafakari!
Kuna mprofesa wengine walienda kusoma Urusi kwa ktumia Kirusi. Wamekuja Tanzania wanafundisha kwa ktumia Kiingereza. Sasa tofauti iko wapi kwa huyo huyo akasome kwa lugha nyingine yeyote halafu aje kufundisha kwa Kiswahili??? Tuache kubweteka, tufikiri kwa undani.
ReplyDeleteWamarekani wamechukua taaluma kutoka kwa Warusi wakatafasiri kwa Kiingereza wanaenda mbele, hivyo hivyo kwa Warusi wamechukua taaluma ambazo hawana lakini ziko lugha zingine ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kichina, Kijapani, n.k., wakatafasiri kwa Kirusi wanatumia na mambo yanakwenda.
Siye hapa tunakaririshwa tuuuuuuuu??? Na nchi haiendi kama imepigwa breki.
Wadau,
ReplyDeleteKwenye elimu kuna madaraja. Kwa mjadala huu tuseme hadi form 4 ni daraja la chini. Form 6 hadi degree ni daraja la kati. Na masters, phd, uprofesa ni daraja la juu.
Kama tutaweza kusomesha kwa kiswahili daraja la chini na kati tutakuwa ni taifa lenye uelewa mkubwa sana. Kwa mfano, asilimia kubwa ya wanafunzi wanaomaliza f4 hawajui kitu katika biologia, fizikia na kemia wanazotumia kila siku katika maisha yao kwa sababu ya kufunzwa kwa kiingereza.
Hili daraja la juu tunaweza kuwalazimisha kusoma kwa kiingereza kwa sababu sio muhimu kwa maisha ya kila siku, na pia wanahitaji rejea (references) nyingi na za hali ya juu ambazo zinapatikana kwa kiingereza zaidi
Maendeleo hayaji kwa kuongea Lugha nyie watu mnaoamini kiswahili kikitumika nchi itaendelea...
ReplyDeleteHivi maamuzi yote yanayofanywa na waafrika ambayo si ya kuleta maendeleo ni kwa sababu ya kutumia lugha ya kiingereza...
Hivi RUSHWA ambayo tunayo hapa kwetu..watu wanakula kwa sababu ya kutumia kiingereza...
Maaendeleo yanaletwa kwa kutumia mbinu za kiuchumi, kisanyansi na teknologia vizuri...kwa ufupi kuzalisha mali kutokana na malighafi.
Hivi tunavyoshindwa kukusanya kodi kutokana na kuendekeza kupewa rushwa ni kwa sababu ya lugha...
Mi uwa naona kuna tatizo..watu wanaopenda kiswahili kitumike wengi wao hawaangalia mambo ya msingi yanayoendeleza nchi...
Nchi zote wanazotaja kama Japan, china, Ujerumani, scandinavia/nordic..watu wanafanya kazi, wanatumia ujuzi, wanazalisha...sisi hatuzalishi bali tunaimport kutoka nchi za nje na tena foreign currency tunayotumia most of it ni ile government inayopata kutokana na kusaidiwa bajeti yake na mkuliwa wa chini akiuza raw cash crops nje....
INABIDI TUWE NA AKILI JAMANI..TUACHA KUFIKIRIA KISIASA..NA KWA KUTUMIA HISIA...TUSOME VITABU NA KUJUA NCHI ZA NJE ZIMEENDELEA VIPI...TUACHE BLABLAA!!