Home
Unlabelled
kutoka maktaba ya globu ya jamii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hivi sasa hao wapo wapi?
ReplyDeleteKutokana na Ukoma na Kansa mbaya sana ya kutothamini Mchango wa Kitaaluma tiliyonayo nchini, kama uhai wao ungalipo hao wakinusurika utakuta wapo ktk Fani kama:
1.Ufundi Baisikeli
2.Uganga wa Kienyeji
3.Ukaanga samaki
4.Kuziba pancha matairi ya magari
5.Kutumbuiza Sarakasi ktk Mabaa
6.Wanacheza Komedi za ktk Mabaa
7.Makondakita wa Daladala
8.Madereva wa Bodaboda
9.Umachinga
10.Udalali wa vyumba na nyumba
11.Ufundi simu kwa kutumia Kompyuta
Hili ni janga la Taifa!
Maoni yako nayaunga mkono ni kweli kabisa hawathaminiwi. Inawezekana kabisa wakawa wanajishughulisha na moja kati ya shughuli ulizozitaja.
ReplyDeleteHii sio Tanzania ya zamani kwamba hiki ni chakwetu, imebaki hiki ni changu
Tuwe macho huko nchi inapoelekea siko
Wewe # 1,umekulia kwenye familia yenye "Neema" hey? .Hayo makundi uliyoyataja naona kama hujayatendea haki,umeyadhalilisha.Mheshimiwa naomba ama ufute kauli yako au utoe ushahidi wa kuthibitisha madai yako.Blog ya jamii,naomba kuwasilisha.Asante
ReplyDeleteDavid V
Ankal,
ReplyDeleteHii haikuwa mwaka 1983 ilikuwa mapema zaidi ya hapo. Kwanini nasema hivyo?
1. Mwaka 1983 mwendo wa 'Chou en Lai' ulikuwa ushakwisha; hata mwalimu naye hakuwa anavaa vazi hilo tena. Hii ilikuwa mapema miaka ya 70.
2. Huyo 'kijana' aliye mbele kama sikosei anaitwa 'Rajabu.' Mwaka 1983 tayari alikuwa kiongozi kikundi cha taifa cha sarakasi. Hebu mtafute bw mmoja anaitwa Issa Sarakasi (sijui kama bado yupo idara ua Utamaduni) yeye atakuwa na data zote.
Ahsante
Ankal,
ReplyDeleteHii haikuwa mwaka 1983 ilikuwa mapema zaidi ya hapo. Kwanini nasema hivyo?
1. Mwaka 1983 mwendo wa 'Chou en Lai' ulikuwa ushakwisha; hata mwalimu naye hakuwa anavaa vazi hilo tena. Hii ilikuwa mapema miaka ya 70.
2. Huyo 'kijana' aliye mbele kama sikosei anaitwa 'Rajabu.' Mwaka 1983 tayari alikuwa kiongozi kikundi cha taifa cha sarakasi. Hebu mtafute bw mmoja anaitwa Issa Sarakasi (sijui kama bado yupo idara ua Utamaduni) yeye atakuwa na data zote.
Ahsante
Wanashuka bandarini kutokea China?! Walienda China kwa boti?
ReplyDeleteAnkali naomba mwenye sanduku hama hayo hapo aniuzie niyaweke kama kumbukumbu
ReplyDeleteMsemaji hapo juu hajadanganya.Maana sanaa hapa kwetu haitiliwi maanani.
ReplyDeleteNi kweli, watu hawa hawakuendelezwa. nakumbuka mmojawapo ni ndugu yangu alienda china kwa sanaa hiyo, sasa anachonga vinyago.Lakini anajivunia kwenda china.
Wakati ule usafiri hadi China ilikuwa ni week 2
ReplyDeletesafari ya kwenda china ilikuwa kwa meli duhh itakuwa imechukua miezi mingapi??
ReplyDeleteumeziona chun lie...hizo
ReplyDeleteNaunga mkono hoja za wadau wote hapo juu na inasikitisha sana. Tanzania hatujali wala kuthamini kazi, vipaji wala uhodari wa watu wetu kabisaaa!. Serikali haina hata mahala pa kuweka kumbukumbu na kufuatilia nyenendo za watu wake mashuhuri na hakuna hata mfuko wa kuwasaidia hili ni JANGA LA TAIFA KAMA ALIVYOSEMA MSEMAJI ALIYETANGULIA.
ReplyDeleteKuna siku nilikuwa pale Benjamin Mkapa Tower kwa kweli sikuamini nilipomuona JELA MTAGWA akipita pale akienda kuomba. Jamani mtu ambaye aliwekwa kwenye STAMP hakuna hata kifuta jasho? Kila STAMP iliyouzwa ilipaswa apate walau kidogo hakuna kitu jamaa anaomba nadhani alikuwa anaenda kwa DAU wa NSSF kuomba inasikitisha sana.
Si kwenye mpira, cinema wala ngoma hakuna lolote. Mzee Morris Nyunyusa tunamkumbuka vipi? tunaenzi vipi kipaji kile?, sisi wa miaka ile tulishazoea kusikia ngoma zake tunajua taarifa ya habari hiyo amefaidika nini? Hili ni JANGA LA TAIFA, tunawakumbuka WANASIASA tu? vipaji vyetu je!
Leonard Tenga hebu chukua changamoto hii na usaidie wachezaji wenzako wa enzi hizo usiwatupe na serikali iweke fungu iwe inasaidia wale wenye hali mbaya kiuchumi. Si wanalipa kodi wale?, hawana viinua mgongo?
Kama sikosei hii haikuwa 1983 bali ni 1969 au mwanzoni mwa 70s. Kama hawa vijana wenzangu bado wapo kila mmoja atakuwa kiasi ya miaka 60.
ReplyDeleteNakumbuka kwenye mwaka 1965 Wachina walikuja nchini kufanya maonyesho ya biashara na utamaduni. Maonyesho yao walifanyika Mnazi mmoja kwenye uwanja wa Kidongochekundu.
Walipoondoka wakatoa offer kwa serikali kupeleka vijana kwenda China kwa miaka 5 kujifunza fani ya sarakasi. Mimi mwenyewe nilitamani kwenda lakini kwa bahati NZURI sikuwahi kufanikiwa.
DAVID V,
ReplyDeleteKiongozi umejibiwa Maswali yako na Anony wa: (8)
......................
Msemaji hapo juu hajadanganya.Maana sanaa hapa kwetu haitiliwi maanani.
Ni kweli, watu hawa hawakuendelezwa. nakumbuka mmojawapo ni ndugu yangu alienda china kwa sanaa hiyo, sasa anachonga vinyago.Lakini anajivunia kwenda china.
............................
Na pia Anymoua wa (12)
Naunga mkono hoja za wadau wote hapo juu na inasikitisha sana. Tanzania hatujali wala kuthamini kazi, vipaji wala uhodari wa watu wetu kabisaaa!. Serikali haina hata mahala pa kuweka kumbukumbu na kufuatilia nyenendo za watu wake mashuhuri na hakuna hata mfuko wa kuwasaidia hili ni JANGA LA TAIFA KAMA ALIVYOSEMA MSEMAJI ALIYETANGULIA.
Kuna siku nilikuwa pale Benjamin Mkapa Tower kwa kweli sikuamini nilipomuona JELA MTAGWA akipita pale akienda kuomba. Jamani mtu ambaye aliwekwa kwenye STAMP hakuna hata kifuta jasho? Kila STAMP iliyouzwa ilipaswa apate walau kidogo hakuna kitu jamaa anaomba nadhani alikuwa anaenda kwa DAU wa NSSF kuomba inasikitisha sana.
Si kwenye mpira, cinema wala ngoma hakuna lolote. Mzee Morris Nyunyusa tunamkumbuka vipi? tunaenzi vipi kipaji kile?, sisi wa miaka ile tulishazoea kusikia ngoma zake tunajua taarifa ya habari hiyo amefaidika nini? Hili ni JANGA LA TAIFA, tunawakumbuka WANASIASA tu? vipaji vyetu je!
Leonard Tenga hebu chukua changamoto hii na usaidie wachezaji wenzako wa enzi hizo usiwatupe na serikali iweke fungu iwe inasaidia wale wenye hali mbaya kiuchumi. Si wanalipa kodi wale?, hawana viinua mgongo?
............................
HIVYO SIFUTI KAULI YANGU, TENA NAKUONGEZEA USHAHIDI MWINGINE HAPA CHINI:
1.Mwinga Mwanjala (Sasa anaishi Milwaukee-Marekani),
Alikuwa Mwanariadha wa Tanzania wa Kike alipeperusha vyema Bendera ya Tanzania kwa kuleta MEDALI ZA DHAHABU na KUVUNJA REKODI mara nyingi tu.
2.Mosi Ally (Sasa anaishi Norway),
Alikuwa mwanariadha wa kike wa Tanzania na aliipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuleta MEDALI ZA DHAHABU na KUVUNJA REKODI nyingi tu.
LAKINI CHA AJABU KUTOKANA NA UKOMA NA KENSA HIYO, WALIKUJA NCHINI TANZANIA KWA VIPINDI TOFAUTI WAKAENDA HADI OFISI ZA RT (RIADHA TANZANIA) ambako kwa MSHANGAO MKUBWA HAWAKUONA REKODI ZAO HATA KTK KAUNTA BOOK WALA ANGALAU DAFTARI LOLOTE LA OFISI HIZO!!!
SASA ITAKUJA KUWA HAO WANASARAKASI?
Kama nilivyoombwa,, naifuta kauli yangu, kama imeeleweka kudhalilisha baadhi ya kazi.
ReplyDeleteJe kwa taaluma walizokuwa nazo wanastahili kuomba? Tusikimbilie kusema sijui wasaidiwe..... sijui wafanyiwe hiki...!
ReplyDeleteJambo la msingi la kujiuliza je wale walioko kwenye fani saa hizi baada ya kuona uzoefu huo sisi tunaotoa maoni haya tuna mchango gani ili kuhakikisha wale walioko kwenye fani saa hizi hawaishii hapo Je tumejiwekea utaratibu wa kuhakikisha hali hiyo haiendelei? badala ya kuendelea kulaumu tuuuu..
Kuendelea kulaumu hakulisaidii taifa letu jamani.
TENGA, Umesikia hiyo mzee!
ReplyDeleteIlikuwa mawka 1970 ndio waliludi kutoka china na meli kwa kuwa baharini kwa siku 21, na kikundi kilivunywa na bunge la taifa mwaka 1982 wote kupelekwa mikoani na wilayani kuwa maafisa wa zaidizi wa wilaya na mkoa baada ya vyeti vyo kuja kutoka China na serikali ilishindwa kukubaliana navyo kimshaara,
ReplyDelete