Meneja wa Miradi Maalum ya mji wa Valejo,California, Bibi Lilibeth Defiesta Asera amehimiza kuwepo kwa mahusiano zaidi kati ya miji ya Valejo na Bagamoyo ambayo yatakuwa na tija hasa kwa upande wa Bagamoyo kutokana na ukweli kwamba mahusiano kati ya miji hiyo miwili ni ya zaidi ya miaka kumi sasa.
Mahusiano kati ya miji hiyo miwili yaliasisiwa na Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwa na wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Bibi Asera anakumbuka namna Mhe.Rais Kikwete alivyotembelea mji wa Valejo na kupata mapokezi ya aina yake na kuelza kwamba wakati umefika sasa kwa mji wa Bagamoja kueleza "Mahitaji yake Mahususi"ili uongozi wa mji wa Valejo uweze kuyafanyia kazi. Alitaja maeneo hayo kuwa ni katika sekta ya uchumi,elimu,afya na teknolojia ya kisasa. Katika ziara yake hiyo ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC, Bibi Asiera alihakikishiwa kufikishiwa ujumbe wake huo kwa uongozi wa mji wa Bagamoyo ili mawasilianzo ya haraka yafanyike.
Pichani juu ni Bw,Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC akimkaribisha Bibi Lilibeth Asera Tanzania House ambaye alikuwa na furaha ya pekee kutembelea Ubalozi huo
|
Home
Unlabelled
mahusiano zaidi kati ya mji dada wa bagamoyo wa valejo wa marekani yahimizwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...