KAMATI ya Ufundi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimetangaza kuanza kwa Ligi ya vijana walio chini ya umri wa miaka 15, itakayoanza Julai 29 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Ufundi wa DRFA, Joseph Kanakamfumu, alisema jana baada ya kikao cha kamati hiyo, kilichokutana jana (Jumapili) kwenye Ukumbi wa Harbours Club Kurasini kuwa ligi hiyo ni moja ya mikakati ya chama hicho katika kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam unaibua vipaji kwa faida ya mkoa na Taifa.

Ligi hiyo itakuwa na faida kubwa kutokana na kuenda sawa na umri unaotumika na mashindano ya vijana ya Copa Coca Cola, ambayo mwaka huu yameanza kwa kushirikisha umri wa miaka 15.

Pia alisema ligi ya wanawake itaanza Agosti mwaka huu huku akiomba wadhamini nao kujitokeza kusaidia ligi hizo.

Wakati huo huo fomu kwa ajili ya kozi ya waamuzi na ile ya mpira wa miguu kwa ngazi ya cheti cha pili  (Inter-Mediate) na  zinapatikana kwenye ofisi za vyama vya mpira vya wilaya vya IDFA, KIFA na  TEFA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...