Mwenyekiti wa jumuia ya watanzania wasabato walioko Marekani iitwayo Tanzania Adventists in the United States (TAUS), Bwana Jeoffrey Ngullu, amewatangazia watanzania wote kwamba mkutano mkuu wa kiroho kwa mwaka umekaribia.
Bwana Ngullu, aishie Philadephia, jimbo la Pennsylvania, amesema kufuatia kufana kwa mkutano wa mwaka jana ulifanyika Washington D.C, uongozi wa TAUS umeamua mkutano wa mwaka huu (TAUS Retreat 2013) ufanyike Houston TX. TAUS inawaalika wote kujumuika, kufahamiana na kujifunza pamoja.
TAREHE ZA MKUTANO: Julai 11-14, 2013
MAHALI- Oak SDA School, 11735 Grant Road, HOUSTON, TEXAS 77429 USA
MGENI RASMI: Mchungaji Lucas Nzungu wa Arusha University, Tanzania
Gharama za mkutano ufikapo TX- ikiwemo chakula, usafiri na hoteli (Holiday Inn)- ni $292.50 kwa mtu aliye tayari ku’share’ chumba (double bed). Kwa wanaotaka chumba cha pekee jumla yao ni $465. Kuna wafadhili kadhaa TX wanaoweza kusaidia gharama za malazi, usafiri na chakula ufikapo Houston. Tafadhali wafahamishe mapema kama utahitaji ufadhili huo.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na mmoja wa wafuatao- Msafiri Lugoe (TX) 281-760-6805; Jeoffrey Ngullu (PA) 267-582-6276; au Shukrani Magoma (DC) 202-607-1976. Asanteni sana na mnakaribibishwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...