Na Abdulaziz video,lindi
Ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari
Tanzania (UMISSETA) mkoani Lindi umefanyika rasmi leo katika Viwanja
vya shule ya sekondari Lindi.
Uzinduzi huo wa michezo ya Umiseta iliyojumuisha wanamichezo 640
kutoka katika Halmashauri 6 za Wilaya zinazounda Mkoa wa Lindi ambapo
mashindano hayo ya michezo hiyo yanafanyika kwa siku nne mfululizo
huku yakitoa fursa ya kuchagua wanamichezo watakaoshiri katika michezo
hiyo Kanda ya Kusini.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Ambae pia ni afisa elimu Taaluma Mkoa
wa Lindi,Sarufu Kakama amesisitiza wanamichezo wote kucheza na
kushindana bila kuumizana na kucheza kwa upendo na kuzingatia nidhamu
kama ambavyo wawapo mashuleni mwao ili kujenga mshikamano baina ya wao
kwa wao ikiwemo na walimu wao.
Aidha Kakama alieleza mkoa wa Lindi ulivyojipanga katika michuano hiyo
iliyoanza leo ngazi ya mkoa kuelekea kanda itakayofanyika Hivi
karibuni mkoani humo
Nae Kaimu Afisa Utamaduni Manispaa ya Lindi,Mwl Alice Choaji licha ya
kuelezea michezo kama masomo mengineyo na kwa kuzingatia somo hilo
kwasababu michezo ni ajira, michezo hutatua migogoro katika jamii
mbalimbali, michezo hudumisha utamaduni wa nchi na makabila mbalimbali
ikiwemo kuibua vipaji vya watoto alieleza.
Katika mashindano hayo kuna jumla ya michezo saba ikiwemo soka wavulana na
wasichana, netiboli kwa wasichana, riadha wavulana na wasichana
kuanzia mita 100 hadi 5000, basketiboli wavulana na wasichana, wavu
wavulana na wasichan na tufe ambapo michezo hiyo itakuwa kifanyika
kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi 11:30 jioni kwenye viwanja hivyo vya
Lindi Sekondari na Mtanda kwa Mpira wa Miguu
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Ambae pia ni afisa elimu Taaluma Mkoa wa Lindi,Sarufu Kakama
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo akipiga penati kuzindua rasmi michuano hiyo
Sehemu ya wanamichezo 640 kutoka katika Halmashauri 6 za Wilaya zinazounda Mkoa wa Lindi
Patashika katika Volleyball
Spike za nguvu mchezoni
Kinadada katika netball


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...