Mahmoud Ahmad,Arusha

Makamu wa kwanza wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar(SMZ),Seif Sharif Hamad ametamka ya kwamba tukio la shambulio la bomu lililorushwa katika kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi na kuua watu watano huku 60 wakijeruhiwa lisitumike kama kigezo cha kuwagawa watanzania kwa misingi yao waliyojiwekea.

Makamu huyo wa kwanza alitoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea eneo la tukio hilo sanjari na kupata fursa ya kutoa mkono wa pole kwa majeruhi mbalimbali waliolazwa katika hospitali ya mkoa ya Mt Meru.

Alisema kwamba tukio hilo ni la kusikitisha ila lisitumike kama njia ya kuwagawa watu kwa misingi yao ya dini na kabila.

Alisema kuwa kila mtu ana haki ya kuabudu dini yake bila kuvunja sheria wala kubugudhiwa kwa namna yoyote.

“Kila mtu ana haki ya kuabudu dini yake bila kuvunja sheria wala kubugudhiwa”alisema Hamad

Hatahivyo,alitoa wito kwa watu wenye taarifa mbalimbali kushirikiana na vyombo vya ulinzi kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa watuhumiwa.

Aliwataka wafuasi wa dini mbalimbali sanjari na wanasiasa nchini kutotumia mwanya wa tukio hilo kuleta mgawanyiko ndani ya jamii.

Katika hatuia nyingine meya wa jiji la Arusha,Gaudence Lyimo alisema kuwa tukio hilo litaathiri sekta ya utalii kwa ujumla na uchumi wa mkoa wa Arusha sanjari na wa taifa kw aujumla.

Lyimo,alitoa kauli hiyo wakati uongozi wa jiji la Arusha wakiwemo madiwani wa vyama tofauti mara walipotembelea hospitali ya St Elizabeth kukabidhi misaada ya mablanketi pamoja na fedha ambazo hakuwa tayari kutaja ni kiasi gani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2013

    Muda mwengine watu tunatakiwa kweli tusifikirie mgawanyiko na tupeane nafasi ya kuabudu dini zetu kwa Amani, ila watu wamepoTeza maisha tunatakiwa kuwafikiria familia zao na kujali familia zao na kujijali nchi yetu kwanza suala la sijui Utalii unapungua kisa ndio tunapopatia pesa tuliweke pembeni na tuachane nayo kabisa uhai wa binadamu muhimu tusipende kuchocheza vitu bila msingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...