Wadau hebu angalieni hii,maana hata haifahamini ni kwanini huyu mwenye gari hii aliamua kuweka gari yake namna hii na kuzuia magari mengine kupita.sasa sijui alikuwa anaharakishia wapi??hapa ni katika Barabara ya Bagamoyo eneo la Lugano.
Mwingine huyu.
ona msururu huu....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2013

    Hivi barabara ya kutokea mwenge hadi tegeta nidhamu itarudi lini? maana ukiangalia chanzo cha msongamano ni watu kukosa ustaarabu na "kutanua" kitu kinachosababisha foleni isiyo na ulazima..hasa wenzetu wenye daladala ndio kabisa yani utafikiri wana sheria zao. Pia maeneo ya jeshini lugalo ndio kabisa maana nakumbuka kipindi cha nyuma pale watu ndio walikuwa wakipita tena kwa nidhamu ya hali ya juu lakini leo hii watu hufikia hatua ya kutanua hata kama kuna MP . Mimi rai yangu ni kwa wenzetu wa jeshi kutoa mfano pale kwa wavunjaji sheria na wanaodharau mamlaka za jeshi ili iwe mfano kwa wengine maana wengine huaribu hata miundo mbinu ya jeshi na kuleta usumbufu usio wa lazima.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2013

    Natumai wahusika na sheria za usalama barabarani wanapitia katika mtandao huu na hatua kali watachukua dhidi ya hawa wavunja sheria. Naomba usichoke kuanika uovu huu katika mtandao na kuhimiza waandishi wengine waige mfano wako. Sio katika mitandao tu, uovu huu wa barabarani uwekwe pia katika magazeti. Labda wakiona wanaanikwa hadharani watakoma. Namba zao za magari ziandikwe pia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2013

    HERI KUTEMBEA KWA MGUU UTAFIKA MAPEMA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2013

    Ubinafsi, kufuata sheria bila shuruti. Hii foleni ya chini wengi ni wastaarabu, lakini picha za juu nkuna wakororofi wasio wastaarabu, wanatanua! na wanajiona wajanja wakati wao wamechelewa kuamka lakini wanataka wawapite waliowahi kuamka, hapana, wadhibitiwe mahayawani hao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...