Na Abdulaziz Video,Lindi
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi Abdalah Ulega amewataka viongozi na
watendaji wa tarafa, kata na vijiji kushirikisha jamii katika
kuzitafutia ufumbuzi kezo zinazowakabili wananchi katika mazingira
yao.
Ulega alisema kero hizo ambazo ni Upatikanaji wa huduma za kijamii
pamoja na migogoro ya ardhi ambayo ikipatiwa ufumbuzi inasaidia
chama cha mapinduzi kuendelea kuaminika kwa Wananchi
Ulega alitoa wito huo wakati alipokuwa anazungumza na viongozi wa
serikali ya kijiji cha Mtoni wilaya humo kwenye ziara ya kuangalia
miradi katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi
"Si vyema viongozi kuchukua uamuzi bila ya kushirikisha wananchi,
badala yake matakwa ya wananchi ndiyo yatumike katika kufanya
maamuzi ya kupanga mipango yote ya maendeleo na utekelezaji wake
wakashirikishwa vyema kupitia vikao muhimu na vya
kisheria...Alibainisha Ulega.
Mkuu huyo wa wilaya alisema hayo baada ya kutembelea zahanati ya
kijiji hicho na kukuta hakuna choo cha wagonjwa na wahudumu hali
ambayo ilimuuzunisha na kuwataka viongozi wa kijiji kwa kushirikiana
na wananchi kuhakikisha choo hicho kinajengwa mara moja.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa choo hicho kutapunguza usumbufu kwa
wagonjwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya kupata tiba na wauguzi
wanaofanya kazi katika zanahanati hiyo.
“Ni aibu kubwa kwenye zahanati mzuri kama hii ikakosa choo kwa ajili
ya wagonjwa na wahudumu hali inayotia aibu kutokana na wahudumu wa
Afya badala ya kufanya kazi wanaangaikia kwenda porini kujisaidia
alimaliziaUlega
Katika ziara hizo za kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya
Kilwa wananchi walitakiwa kutambua kuwa miradi yote ya maendeleo
inayotekelezwa katika vijiji vyao ni mali yao si ya serikali hivyo ni
wajibu wao kuitekeleza kwa wakati na pindi ikamilikapo ikatunzwa
ipasavyo
samahani kaka Michuzi nina swali linanisumbua siku nyingi naamini utanisaidia. Hivi vest si ni nguo ya ndani? Hii syle wanume mmeitoa wapi jamani?
ReplyDelete