Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Kelvin Albert (3) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo.
Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Deric Siprian Kessy (8) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto kwa Makamu ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo na (kulia) kwa Makamu wa Ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Alex Malasusa.
Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Gabriel Godfrey (9) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Restuta Alex (50) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa mahututi, aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, wakati alipowasili nyumbani kwa askofu huyo jijini Arusha jana kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha kwenye hafla ya uzinduzi wa Kanisa hilo.
Mamaku wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa papa Francis, Askofu Francisco Montecillo, walipokutana nyumbani kwa Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, alipofika kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha. Picha na OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2013

    OMG Where are we heading? God forbide

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2013

    wadanganyika tujiulize toka lini nchi yetu ilikuwa na mabala kama haya na kwa nini yawepo tusiwe wapokea habari na wasomaji tu wa mablog bila kukaa chini na kufikiri na kutafakari tusiwe watumwa wa kushindwa kutumia akili zetu muumba aliyetujalia kuwa nazo tusizarau haya matukio yanayotutokea tujiulize chanzo chake nini na kwa nini, hivi kweli watanzania watanganyika tuna tabia hizi za kujirupua ripua na kuwaripua watu

    tukaeni chini tutafakari kwa kina cha urefu usio na mfano other wise taifa linakwenda mrama

    masikini TANZANIA YETU, TANGANYIKA YETU ENYI WADANGANYIKA TUFIKIRI TUSIWE WATUMWA WA KUSHINDWA KUFIKIRI NA KUJISOMEA VIJIHABARI VYA HAPA NA PALE

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2013

    HIVI JAMANI TUNAELEKEA WAPI?????TUJIULIZE .TUSIJE TUKAWA WAJINGA KAMA WENZETU WANAOUANA TOKA ENZI ZA MITUME BILA KUPATA SULUHISHO
    TUSIJEWAFANYA WAPENDA AMANI WAKALIA NA KUTAFUTA MAKAZI NCHI ZA JIRANI KISA HATUJUI
    MUNGU WETU NI MMOJA HATA AKIITWA GOD.AU MOLA ATAKUA NI MUNGU
    T
    AKIJULIKANA ALOFANYA LAZMA ATESWE IWE FUNDISHO

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2013

    ndo kiyama hicho tanzania na watanzania hatuna mila hizi za kujiripuo so kaaeni tayari kujua kiyama hakipo mbali

    poleni sana wafiwa wote na ndugu na jamaa wote watanzania wenzangu

    kiama hicho je mmejitayarishaje kumuona muumbwa wenu siku za mwisho ndo hizi subirini anti chris aje(dajad)

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 07, 2013

    unadhani watu wa zamani enzi za mitume walikuwa wajinga? wewe mdau wa mwisho watch what you write usije na jazba zako hapa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 07, 2013

    Hakuna kitu hapa ni mipango tu ya wenyewe. Jamani ndugu zangu, siku zote ukiona tabia fulani ktk jamii imeshindikana kudhibitiwa ujue kuna kigogo nyuma yake... Angalieni fujo za barabarani. Maderevahawafuati kabisa sheria za barabara .Ajali kibao . Kelele zimepigwa weeeee kukomesha lakini wapi . Kumbe wenye magari madogo, pikipiki, bodaboda, daladala, hata mabasi makubwa ni maaskari wa vyeo, mawaziri na wabunge.

    Nahii ya mabomu iangaliwe.. sijui na nani?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 07, 2013

    Ule mwanga wa Tanzania ni kisiwa cha amani sasa unazimika; bila shaka. Viongozi, wananchi tafakarini sana nini maana ya ugaidi na niwepi magaidi au ni imani ipi ni ya kigaidi.

    Nivizuri pia tukaangaza upya juu ya vikosi vya TZ kuingia vitani dhidi ya M23 huko Congo DRC. Yawezekana ni honi hiyo bado gari kupita.Tujiandae.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...