Bw. Nkosinathi Nxumalo, anayemnadi Mfalme Mswati wa Tatu popote aendapo. Huyu msanii alitia fora sana katika maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Kama inavyoonesha video hapo juu, yeye  kazi yake ni kuongozana na Mfalme huyo kila aendako na kumnadi mbele ya watu anapowasili mahali popote kwa sauti ya juu katika kudimisha mila na utamaduni wa nchi hiyo ya Kifalme. 
Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa  Balozi  Tuvako Manongi  akiongea na Bw. Nxumalo baada ya kuvutiwa na kazi yake ya kumnadi Mfalme Mswati wa Tatu wa Swaziland.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2013

    that's why africa will be 3rd world for so many years ahead.

    J4
    ujerumani

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2013

    Duh! Hata JK ameachwa hoi. Sijui Bagamoyo hakuna vitu kama hivi nini? Any way, hizi mila za kuutukuza utukufu wa binaadamu kiasi hiki hazipitani sana na utumwa. Ila mdharau mila pia ni mtumwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2013

    Anonymous wa kwanza hii siyo Africa tu. Rais wa Marekani anapoingia mahali buruji huwa linapulizwa kuimba hear comes the chief. Tuache hii tabia ya kudharau vitu vya kwetu.
    Viongozi huwa wanatangazwa wanapoingia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2013

    Hiki kigezo cha kutumwisha watu hakina akili.

    Mkataa mila awa mtumwa, haya we uliye huru katahiri wanawake.

    Mkataa kwao mtumwa, babu yako mkongo unafanya nini tanganyika?

    Kwao mtu ni pale alipochagua, huo ndo uhuru.

    Hii mijitu sijui haisomi DS?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2013

    Inawezekana Kijana Mwakilishi wa Mswati III amevutiwa zaidi na kale Kasherehe anakofanyiwa Muswati mwenyewe kila mwaka halafu anachagua TOTOZ mpya!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2013

    wadau mliotangulia hapo juu siwezi kusema mmekosea kwakuwa kutoa maoni ni haki ya kila mmoja wetu

    nafikiri hili tukio ni zuri sana na limependezesha sana na kutufanya tujivunie uafrika wetu

    ninajuwa asilimia kubwa ya wenzetu wanaoishi ughaibuni wanapenda ingelikuwa afrika ya leo kama ulaya

    lakini mkae mkifahamu afrika tutabaki kuwa afrika na waafrika wake na sio wazungu

    mambo ya kuiga kwa wazungu sio kila jambo linafaa kuigwa

    jamaa kapendeza na vazi lake asilia na vile vile kapendeza zaidi kwa lugha yake asilia

    sisi tutabaki kuvaa suti kuiga mavazi ya watu na lugha za watu hali ya kuwa hatujui vazi la taifa ni lipi

    safi sana ankali nimeipenda sana hii ningelipenda kuona mengi kama haya.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2013

    DUMISHA MILA ZAKO Usithamini na kudumisha za wakoloni na kudharau zako. Hongera Mswati

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2013

    Nimeipenda sana hii

    na sisi inatakiwa kuiga mila za hawa wa Swazi

    Kama wananchi wao wameridhia why not?

    sioni ubaya wowote ule.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2013

    This is pathetic. Look at the stooges who are dressed in western GURB: wajiona wameshafika. Na kama sikukosea wana mcheka Mswazi alo-vaa kitamaduni.

    This at least 50 years baada ya uhuru among most sub-saharan so called western labelled countries; na waheshimiwa hawaja-amka. Bwana "kama hujui asili yako na ulikotoka:sidhani utakua na uewezo wa kuona zaidi ya pua yako.Jamani mbona tuna kaazi!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 27, 2013

    michuzi comment yangu imebaniwa nitairudia bila kuvunja heshima kwa kifupi big up Swaziland kwa kudumisha mila wanaokucheka ni watumwa Africa tudumishe mila zetu popote tunapoenda tusifate ya magharibi wenyewe wameshajichanganya hata hawajijui tena wananchi dumisha mila zetu popote ulipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...