Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada,  Mhe. John Baird  alipowasili kwenye Hoteli ya HyattyRegency Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki Chakula cha Mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Membe. Mhe. Baird alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine pia walizungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Canada pamoja na kusaini Mkataba "Foreign Investment, Promotion and Protection Agreement" (FIPA).


Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Baird wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu.



Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Baird akimsikiliza. Kushoto ni Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Alexandre Leveque.





Mhe. Membe akimkabidhi Mhe. Baird zawadi ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro. Picha na Rosemary Malale


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...