Na Abdulaziz Video,
Hali ya usalama ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni tete. Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi. Usafiri wa Pikipiki unapatikana katika baadhi ya maeneo machache ya mji, huku maneo makuu ya biashara yakiwa wazi bila ya pilikapilika za watu kama ilivyo kawaida. 
 Polisi wakiwa kwenye magari wameonekana katika maeneo mbalimbali ya mji, na wengine kuweka makambi madogo katika maeneo yanayoaminika kuwa na msongamano wa watu katika siku za kawaida.
Mwandishi huyu ameshuhudia magari ya polisi yakiwa na askari katika maeneo ya Bima, Soko kuu ambako pia kulikuwa na gari la kumwaga maji ya kuwasha, Magomeni, Skoya na Majengo.
 Hata hivyo hadi kufikia saa 7 mchana hakukuwa na hali yeyote ya uvunjifu wa amani, makundi ya vijana walionekana wakijadiliana mambo katika maeneo mengi ya mji. Hali hiyo imejitokeza kufuatia kusambazwa kwa vipeperushi na ujumbe wa simu za mkononi na watu wasiojulikana ukiwataka wafanyabishara kusimamisha shughuli za biashara kwa siku ya (leo) jana ili kutoa fursa kwa wananchi hao kusikiliza bajeti ya Nishati na Madini iliyotarajiwa kuwasilishwa leo Bungeni mjini Dodoma. Hata hivyo bajeti hiyo itawaslishwa Bungeni Mei, 22, mwaka huu. 
 Sehemu ya kipeperushi hicho kilichopambwa na picha ya mtoto aliyeshikia kombora kinasomeka “Wote kwa pamoja siku ya tarehe17.05.2013 (Ijumaa saa 3 asubuhi) tusikilize bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (Bungeni) ili kujua mustakabali mzima wa gesi yetu na ili kuonyesha kilio, msimamo wetu kwa serikali wa kutaka maendeleo kwa mikoa ya kusini, siku hiyo huduma zote za jamii zisimamishwe” 
 Licha ya polisi mkoani hapa kuwasihi wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa jeshi hilo litaimarisha ulinzi bado wananchi wameonesha kutokubaliana na wito huo. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa ameliambia amesema kuwa hali ni shwari na kwamba jeshi lake limeimarisha ulinzi.
 “Hali ni shwari, wapo madereva Bodaboda wanaendelea na kazi zao, wananchi wanatembea kama kawaida, ispokuwa baada ya maduka yamefungwa” alisema Sinzumwa
Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi.
Ulinzi umeimarishwa kila kona
Mji wa Mtwara ni sehemu ya pilika pilika ya watu lakini leo hali si hivyo na katika kituo kikuu cha mabasi cha Mtwara hakuna basi lililoingia au kutoka kutwa nzima leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...