Na Abdulaziz,Lindi
Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Ismai Mayoba(31)anaefanya kazi Bar
ya Mangrove,Mkazi wa Jamhuri, Manispaa ya Lindi, amenusurika kifo baada
ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimaye kumchoma
moto.
Mayoba amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo
Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa
kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa saba wanaosadikwia walihusika na tukio hilo
lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.
Akithibitisha tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa, Afisa
Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja Ally Manially (22) mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi
hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na
kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma
mwenzie Moto huku akijua ni kosa kisheria
Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta
watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo
Taarifa zaidi tutawaletea kuhusiana na tukio hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...