Mkutano unaozungumzia masuala ya uhuru na usalama wa mtandao kwa maendeleo ya Dunia umeaza leo mjini stockholm. Mkutano huo ambao umeandaliwa na Wizara ya mambo ya Nje ya Sweden umefunguliwa leo MEI 22, 2013 na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Hon. Carl Bret.

Mkutano huu muhimu ambao unakutanisha wataalamu wa masuala ya Internet na (policy makers) kutoka nchi zaidi ya Tisini na Tano(95) unazungumzia mambo muhimu kuhusiana na uhuru wa Mtandao ambao unahitaji kulindwa na kuheshimiwa na bila kusahau Usalama wa raia na maendeleo yao.

Mkutano huu wa siku mbili utazungumzia changamoto zilizopo ikiwa na ukweli kwamba kuna baadhi ya serikali za baadhi ya nchi duniani zimekuwa zikitaka kuwa na (control) na maamuzi makubwa kuhusiana na uhuru wa Mtandao(Internet) kwa sababu zao binafsi kwa kisingizio cha usalama au kulinda usalama wa raia.

 Mkutano unajadili mambo ya usalama na sera maalumu ambazo zitakuwa zinakubalika zenye kuheshimu uhuru wa habari.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Hon. Carl Bret akifungua mkutano wa STOCKHOLM INTERNET FORUM ON INTERNET FREEDOM FOR GLOBAL DEVELOPMENT - SIF13.
Bw. Wilfred Warioba akiwa na Fadi Chehadé, na Raisi na CEO wa (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers, ICANN).
Dr. Dorothy Okello form Makerere University and Founder of WOUGNET, Mr. Wilfred Warioba from Commission for Human Rights and Good Governance-Tanzania, Mr. John Ulanga, Executive Director, the Foundation for Civil Society.
Kutoka kushoto Dr. Jabir Bakari, CEO wa e-Governance-Tanzania, Dr. Dorothy Okello form Makerere University and Founder of WOUGNET, Mr. Wilfred Warioba from Commission for Human Rights and Good Governance-Tanzania, Mr. John Ulanga, Executive Director, the Foundation for Civil Society.
Kutoka kushoto Mr. John Ulanga, Executive Director, the Foundation for Civil Society Mr. Wilfred Warioba kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dr. Jabir Bakari, CEO wa e-Governance-Tanzania.
Bw. Warioba kutoka Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Carl Bildt.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2013

    Ningeshangaa kama nisingemwona Dr Bakari Kuwe...!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013

    Oh! Namuona na Nd. Warioba...Kwa kupitia mtandao huu, ninasikitika kuwajulisha kuwa, majembe mengi mliyoacha UCC yalishaondoka kati ya June, 2012 mpaka Dec, 2012. Ni kwa njia ile ile .

    Prof Beda
    Dr Mfuka
    Graham ( alifariki )
    Mesanga
    Athanace
    Vicky
    Mbembati
    Mokiwa



    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Naona vijana wa UCC mnashine kwa kwenda mbele, Hongereni Dr. Jabir Kuwe, Wilfred Warioba..

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2013

    Ucc hutoa product bomba..nimesoma majina ya hawa walioitwa majembe nafahamu mmoja tu alifanya kazi kwa kairuki zamani sana. Habari za kuaminika zinasema ukakamavu wake katika kutimiza majukumu kulisaidia sana ile hospitalikutimiza malengo. Huyu mmama si msomi sana, lakini tendaji wake wa kazi utafikiri amesoma mpaka no class.

    Bahati mbaya wasomi wa fani yake humchukia kinoma kwa sbb hupenda sana kufuata taratibu za kazi, wakati wenzake hupenda kupindisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...