Martin Ngireu Enzi ya Uhai Wake
Familia ya Ngireu inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa baba yao Martin Ngireu kilichotokea siku ya Jumanne May 21, 2013 katika Hospitali ya Holy Cross iliyopo Silver Spring, Maryland, nchini Marekani.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Donalson Funeral Home, iliyopo 313 Talbot Avenue, Laurel MD na kutakua na Misa na kumuaga marehemu siku ya Jumamosi May 25, 2013 kuanzia saa 6 mchana mpaka saa 10 jioni (12-4pm) kwenye addres 313 Talbot Avenue, Laurel, MD baada ya hapo kutakua na chakula kwenye address 210 Patuxent Road, Laurel MD

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inafanywa na kama ilivyodesturi yetu kupena pole ndio ustaarabu wetu Msiba upo 210 Patuxent Road, Laurel MD kwapa pole watoto wa marehemu Carol na dada yake waliokuja kutoka Tanzania. Msiba huu ni wetu sote DMV tafadhali tujumuike na tuwafiriji wafiwa. Kushirikiana na kushikamana kwa shida na raha ndio staili na maisha yetu DMV.
Kwa maelezo na maelekezo tafadhali wasiliana na Mtoto wa Marehemu Carol 301 957 4523.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2013

    ndugu zanguni, poleni sana na matatizo, mwenyezi mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi na mwanga wa milele aingazie; lakini ningeomba kufahamishwa maana ya neno DMV.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2013

    Mie sijichanganyi na Wabongo siji.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2013

    Division of Motor Vehicles. Huku US, ni lazima uwe na ID (kitambulisho) na kinatolewa kutoka DMV. Tatizo la DC ambako kuna watanzania wengi, wanafikiria wao tu ndo wana DMV

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2013

    Maana yake ni DC, Maryland na Virginia.
    Mzozaji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...