Waumini wakiwa katika taharuki kufuatia mlipuko huo wa bomu jijini Arusha leo. Chini makachero wa polisi wakifanya uchunguzi eneo la tukio. Picha na Woinde Shizza
Baba Askofu Mkuu wa Jimbo la Kanisa Katoliki Arusha, Mhashamu Josephat Louis Lebulu na Mwakilishi wa Papa, Nuncio, Francisco Montecillo Padilla kabla ya mlipuko huo. Viongozi hawa wa dini walinusurika na waliondolewa haraka eneo la tukio na wasaidizi wao wakiwa salama

Taharuki mara baada ya mlipuko huo wa bomu

Na Ahmed Mahmoud
MTU mmoja amekamatwa na anaendelea kuhojiwa na polisi kufuatia mlipuko mkubwa wa bomu lililorushwa kwa waumini wa Kanisa Katoliki jana ambapo watu 66 wamejeruhiwa wakiwamo wanawake 41 na wanaume 25, huku majeruhi wawili hali zao zikiwa mbaya zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Magesa Mulongo alimweleza Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Mwema,Naibu waziri wa mambo ya ndani Mhe Pereira Silima,na Naibu Waziri wa Nishati na Madini  Mhe Stephen Masele wakati walipowatembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mount Meru jana jioni.
Alisema kati ya majeruhi hao, wawili hali zao ni mbaya, huku mmoja akiwa akiwa amepelekwa hospitali ya KCMC kwa matibabu zaidi.
Makamu wa Rais alitarajiwa kuondoka na majeruhi mwingine mtoto ambaye anapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
RC Mulongo alithibitisha kwamba aliyefariki katika tukio hilo ni mama mmoja wa kwanya ya Kimasai ambayo ilikuwa ikiimba kwenye shughuli za uzinduzi wa kanisa hilo.
Akitoa pole kwa wagonjwa waliolazwa pia kwa wale ambao jamaa zao wamepata maradhara kwa tukio hilo, kwa waumini wa Kanisa Katoliki, kwa wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla, Dk Bilal alisema tukio hilo ni la aibu na baya sana.
“Tukio hili ni la aibu sana, baya, limeshtusha kutokea hapa nchini, serikali inalaani na itafanya kila linalowezekana kuwatia mbaroni wahusika na tayari imekwishaanza kuhakikisha wahusika wanakamatwa.
“Vyombo vya usalama vimeagizwa kufanya kazi hii usiku na mchana kuhakikisha kwamba wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua,” alisema.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mwema akitokea Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge ambako leo Wizara ya Mambo ya Ndani inawasilisha bajeti yake, alielezea tukio hilo kuwa ni la kushutua sana.
“Ni tukio la kushtua, kusikitisha, tumefika eneo la tukio na mpaka sasa mtu mmoja amekamatwa na anaonyesha ushirikiano mzuri wa kutoa taarifa.
“Tukio kama hili sio la mtu mmoja, wapo waliohusika katika kupanga, kuratibu, kushauri, kuchangia gharama na wale waliofanikisha. Hata huyu mmoja aliyekamatwa ni mchango wa ushirikiano wenu, naombeni muendelee kushirikiana na polisi katika kufanikisha uchunguzi huu.
Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, ambaye aliambatana na Makamu wa Rais kutokea mkoani Shinyanga, alisema amesikitishwa sana na tukio hilo.
Alisema tukio hilo sio la kawaida na limewashtua watu wengi wanaopenda amani lakini amewaomba waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linapoendelea kufanyiwa uchunguzi.
“Wakristo tuendelee kuhubiri amani, kuombea amani kwa sababu Mungu wetu ni wa amani,” alisema.

Majina ya waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospitali za mount Meru, na hospitali teule ya jiji la Arusha ya St Elizabeth wametambulika kuwa ni:- John Thadei, Regina Fredirick, Joram Kisera, Novelt John, Rose Pius, John James, Anna Kessy, Joan Temba, Neema Kihisu, Gloria Tesha, Innocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, Simon Andrew, Anna Edward, Lioba Oswald, Rose Pius, Philemon Gereza,Kisesa Mbaga na Beata Cornell.

Majeruhi wengine na umri wao katika mabano, ni Consensia Mbaga (53), Christopher Raymond (10), Deborah Joachim (24), Elizabeth Isidori (24), Anna Didas (52), Bertha Cosinery (49), Edda Ndowo (77), Derick Cyprian (8), Faustine Andrea (35), Mary Okech, Mesoit Siriri (33), Clenes pius (22), Joyce yohana (15), Restituta Alex (50), Mathias Riha (74), Magreth Andrew(45), James Gabriel (16), Regina James (17),Elizabeth Masawe(15), Elizabeth Sauli (18), Njau (35), Yasinta Msafiri (16) Doreen Pancras (28), Alex Arnold, Agripina Alex (9), James Gabriel (16), Loveness Nelson (17), Amalone Pius (25), Frank Donatus (10), Alphonce Nyalandu (26), Athanasia Reginald (14), Phillemon Ceressa (49), Neema Daud (13), Sophia Kanda (72), Theofrida Innocent (21) na Regina Darnes(17).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2013

    Haya mambo ya ugaidi sidhani kama yametokea tu kutoka kwa wahuni. Ni watu wenye akili na nyazifa zao na wanajulikana hivyo wa TZ tukae makao wa kufa tu ili wabaki wenyewe hao wenye ugaid wao

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2013

    TAZAMENI PICHA VIZURI KABLA HAMJARUKIA CONCLUSION ZA UGAIDI...HIZI PICHA ZINAELEZA MENGI NAOMBA MFUNGUE MACHO YENU KUONA YALIYOMO KWENYE PICHA HUKU MKIHUSISHA NA MRIPUKO WA BOMU..MIMI KUNA MASHAKA NIMEYAONA KATIKA PICHA YAMEACHA MASWALI MENGI KICHWANI MWANGU. TAFADHALI WAHUSIKA WATUMIE WATAALAMU WA KUSOMA HIZI PICHA KUTAZAMA NINI HASA KIMETOKEA NA HIZI PICHA ZINAONYESHA NINI. NATAMBUA WATANZANIA TUKO MBIO KUTAJA MAMBO MAKUBWA BILA KUFIKIRI UZITO WA MANENO TUNAYOYASEMA..BOMU LISILO NA MOSHI WALA MOTO NA WATU WALIOSIMAMA HUKU TOKEO LIKIENDELEA LINANIPA SHAKA. TUNAWEZA KUANZA KUUWANA KWA DHANA POTOFU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2013

    Kwa kweli kama serikali haitokuwa makini na jambo hili tunaendea kubaya, kwani mpaka sasa kwa matukio yote haya yanayohusu makanisa na viongozi wake hakuna hatua yeyote ya maana ambayo imechukuliwa mpaka sasa. Hivyo ndugu zangu tuendelee
    kufunga na kuomba kwa nguvu zetu ili Mwenyezi Mungu atunusuru. Hatuna serikali.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2013

    Naunga mkono mtoa maoni wa kwanza. Kila jambo baya ukiona limeshindikana kudhibitiwa ujue kuna kigogo nyuma yake. Angalia uvunjifu wa sharia za barabara. Kumbe magari mengi ni ya maafande na wakuu wa mikoa na mawaziri.

    Mihadhara ya kukashifu dini. nayo kuwa wenywewe.Mheshimiwa rais kila kukisha analaani na kuwashauri waathirika kuwa na subira. Sawa, tutavuta subira mwisho wa kuvuta subira usije ukageuka kusukuma subira

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2013

    anonymous wa kwanza umesema point kidogo tu nakuunga mkono kwamba hawa watu wi wahuni ni watu wenye akili na nyazifa zao si wahuni kabisa na tujiulize ni wakina nani? na wana niana gani? na cha kushangaza toka lini tanzania tulikuwa na matukio kama haya hivi sasa iweje?

    hivi bomu mnalijua mnalisikia mtanzania wa kawaida kishawahi kulishika, janja ya nyanyi kula mahindi hii kitu kimepangwa na wanajulikana wa wamo humu humu na nyazifa zoa ndo maana utaona matukio yakitokea eti wanakuja waokozi kujitokeza na kukema na kujidai wadini

    tunajua hampendi aliyepo madarakani ndo maana mnamuharibia lakini mungu mkubwa na mwisho wa siku na nyinyi pia mtakufa hatoishi milele na mtakiona cha mtema kuni mbele ya mungu wenu because you will be ask what you did hata kama mkiungama zambi daima hafutiki

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2013

    Mdau wa mwanzo umesema kweli hawa hatu si wahuni na wana nyazifa zao na kitu kimoja cha kusema ni kwamba wanafanya haya ili iweje kwani wao wataishi milele kuna siku wataondoka katika hii dunia na watamjibu mungu wao yote yale waliotenda kuumuuwa mtu mungu hasamehe hata ukimuomba msamaha mara mia so wajiulize tu wataishi mpaka lini na kufanya haya mpaka lini


    majuu huku wamefanya na kufanya mwisho wa siku watu wana soma data zao yote waliowatendea watu weusi etc na wanatoka hadharani kuomba samahani au wengine wanachuna tu lakini guilty eat them alive and god is waiting for them amen

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2013

    wanafanya haya ili serikali isitawalike, ili wahongwe tena kama walivyohongwa kura na wakanyamaza wanataka pesa zitoke ikulu wajinufaishe wanafanya haya kwa sababu hawamtaki mkuu aliyopo wanakisasi kwa ajili walio mtaka alikuwa mzinifu halafu eti mcha mungu wao na akakosa kura

    tunayajua mengi tu watanzania wa kawaida ndo watadanganywa na matukio haya etc

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 07, 2013

    watanzania sio wajinga hatuna kasumba za ujinga kama enzi za hamsini kweusi kutumiwa kama mandondocha na mamluki watanzania tuko imara na waunga mkono wote waliotoa comment zao na zina ukweli wake inaonyesha jinsi watanzania tulivyo wafikiri sio kila kitu tukiandikiwa na kuonyeshewa tunakimeza mara mmoja tunatafakari na kuona mbali

    safi sana japo kuwa tuta kuwa hatuna nguvu au waoga kuiogopa serikali au wahusika fulani ili kulinda riski zetu au maisha yetu na ndugu zetu lakini si wajinga sisi bwana

    angaliyeni kweli picha hizi kama kweli bomu limetumika, wanafanya wenyewe na wakina nani mara nyingi wana mabomu hapa nchini?

    watanzania sio wajinga kama tulivyokuwa huko nyuma

    kazi ipo poleni mliokuwa wamekutoeni mhanga na subirinina bado mpaka wakutoeni roho wote

    lakini GOD IS WATCHING AKIKUTIYENI MKONONI NDO MTAMJUA MUNGU NDO NANI HATA MKISALI SALI NA KULIA LIA NGUVU YA MUNGU IKIPITA MTAKIONA CHENU

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 07, 2013

    Tanzania Tanzania
    Nakupenda kwa moyo wote
    Nchi yangu Tanzania
    Jina lako ni tamu sana
    Nilalapo nakuota wewe
    Niamkapo ni heri mama wee
    Tanzania Tanzania
    Nakupenda kwa moyo wote!!!

    Mungu ibariki Afrika
    Wabariki Viongozi wake
    Hekima Umoja na Amani
    Hizi ni ngao zetu
    Afrika na watu wake.
    Chorus:
    Ibariki Afrika, Ibariki Afrika
    Tubariki watoto wa Afrika.
    Mungu ibariki Tanzania
    Dumisha uhuru na Umoja
    Wake kwa Waume na Watoto
    Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
    Chorus:
    Ibariki Tanzania, Ibariki Tanzania
    Tubariki watoto wa Tanzania.

    Mdau Columbus Ohio

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...