Baadhi ya waombolezaji waliokutwa na mtandao huu nyumbani kwa marehemu Dk. Masau, Mbweni Kwa Jumbe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.  
Imeelezwa kuwa Dk. Ferdinand Masau, aliyefariki jana katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa, anatarajiwa kuugwa kesho hapo hapo katika Hospitali ya Aghakan saa 5:00 asubuhi. 

Baada ya hapo mwili utarudishwa nyumbani kwake kabla ya kusafirishwa keshokutwa kwenda kwa maziko kijijini kwao Murutunguru, Wilaya ya Ukerewe. Picha na GPL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2013

    RIP DOCTOR

    ReplyDelete
  2. R.I.P docta tutakukumbuka sana kwa jitihada zako za kuokoa maisha ya watu hasa sisi, kama mimi hapa niliyepata bahati ya kutibiwa na wewe na kupeleka baadhi ya ndugu kwenye hospital yako tangu ukiwa mikocheni hadi ulipoamia kinondoni kwa kweli ulifanya kazi yako kwa moyo ili kuokoa maisha ya watu nakuombea kwa MUNGU AKUPOKEE MBINGUNI,nakumbuka ulikuwa unawasamehe kabisa kuwachaji wale walioonyesha kushindwa kabisa kulipia gharama bali uliwahudumia waponye naandika hii msg huku nalia kwani niko mbali na tanzania kwa sasa siwezi ata kuja kukuzika wala kukuaga bali jitihada na huduma yako haitakaa initoke ndani ya kumbukumbu ya moyo wangu,
    ULIAMUA KUACHA KAZI KWA HIYARI YAKO NCHINI MAREKANI UKIWA DOCTA BINGWA WA MOYO WAZUNGU WANAKUHESHIMU NA KUKUTUMAINIA UKAAMUA KUJA NCHINI KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA YAPO HUKUPATA SAPOTI LAKINI ULIPIGANA .
    RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE APUMZIKE KWA AMANI AMINA

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2013

    Ndio maana watu wanavunjika moyo kurudi Tanzania.

    Ukifika nyumbani unageuzwa adui.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2013

    Poleni sana familia ya Dr. Masau kwa msiba huu mkubwa. Hakika Dr. alifanya kazi kubwa sana ya kuokoa maisha ya watanzania wengi. Kama mdau alivyosema hapo juu, kwa wasiojiweza aliwasamehe kulipia gharama na kuwatibia bure hiyo ni kweli kabisa. Mbali na hiyo alihakikisha kila anayefika hospitalini anapata huduma yake hata kama saa za kazi zitakuwa zimeisha alihakikisha anawaona wagonjwa wake wote bila kuwarudisha waje siku nyingine! Dr. alikuwa na moyo wa pekee wa kujitolea kwa watanzania ili kuhakikisha wanapata huduma bora za matibabu. Nakumbuka kukutana na wagonjwa toka mikoani pale THI. Na pia support kubwa ya madaktari toka nchi zingine ikiwemo ujerumani walikuwepo kutoa huduma THI sambamba na Dr. Masau. Hakika uliifanya kazi yako kwa moyo wa dhati na kwa hiyari kabisa. Mfano wako Dr. Masau ni wa kuigwa kwa madaktari waliobakia Tanzania.Madaktari wote mngekuwa na moyo kama wa Dr. Masau Tanzania ingefika mbali kwenye sekta hii ya afya ya utabibu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2013

    only the good dies young. RIP doc.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...