Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya
kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame
Silima kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya kisasa ambayo imejengwa
na jeshi hilo, katika Gereza Isanga, mjini Dodoma. Ufunguzi huo umefanyika leo
mjini humo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Pereira Ame Silima akizungumza na maafisa
magereza kabla ya kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya kisasa ya
Jeshi la Magereza ambayo itawawezesha maafisa wa jeshi hilo, askari na familia
zao kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
John Minja na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shops ambaye ndiye
aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Bw. Afzal Meghji.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Supermarket (Duty Free Shop) ya pili ya Jeshi la Magereza
iliyojengwa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Military Shop, Bw. Afzal Meghji akimuonyesha bidhaa mbalimbali
zilizopo ndani ya Duty Free Shop ya Jeshi la Magereza, Isanga mkoani Dodoma, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima (kulia). Kushoto ni Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja.
Baadhi
ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa mbalimbali baada ya kuzinduliwa
kwa Supermakert (Duty Free Shop) ya Jeshi la Magereza iliyopo Isanga, mjini
Dodoma.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (wa katikati waliokaa), Mkuu
wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja, (wa tatu kushoto waliokaa) wakiwa katika
picha ya pamoja na maafisa mbalimbali wa magereza pamoja na wageni waalikwa
baada ya kufungua Supermarket (Duty Free Shop) ya kisasa ya jeshi hilo, mjini
Dodoma.
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Je, mtu wa kawaida anaweza kujinunulia chochote hapo, japo hatuvitengenezi?
ReplyDelete