Na Abdulaziz video/Lindi yetu Blog 
Redd’s Miss Lindi 2013 atajulikana Usiku wa tarehe 31 may,2013 ndani ya ukumbi wa Lindi Beach Resort. Jumla ya Warembo Kumi watachuana Vikali kugombania taji hilo. 
Warembo hao wako kambini Hotelini hapo kwa mazoezi makali huku wakiongozwa na Redd’s Miss Lindi 2012. 
Mratibu wa Mashindano hayo Ndugu Justine alisema Mwaka huu wamejiandaa vizuri na warembo wako katika hali nzuri ya kiafya kambini hapo na Pia anataraji show itakuwa ya Kihistoria kwa jinsi maandalizi yalivyo andaliwa, hivyo amewataka wadau kujitokeza kwa wingi. 
 Viingilio vimetajwa kuwa viti vya kawaida siku hiyo vitakuwa Tsh 10,000/= na VIP itakuwa 15,000/= na tiketi zitaanza kuuzwa siku hiyo hiyo ya tarehe 31/05/2013 majira ya asubuhi Hivyo wahi tiketi yako mapema ili ushuhudie show ya kihistoria katika mambo ya urembo katika mji wa Lindi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2013

    lLAKINI WOTE HAO FROM LINDI ORIGIONAL? HAKUNA MAMLUKI HUMO?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2013

    je wote hao ni watoto wa kimachinga?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2013

    Duhhh kweli kazi ipo Lindi!

    Tutakosa uhondo wa aina yake, si mchezo Mabinti wa Kiungwana wa Kimwambao wa Lindi ndani ya gemu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2013

    Mdau wa kwanza, hapo tena hilo ni suala la muhimu!

    Inawezekana kabisa miongoni mwao wamo mamluki wameshiriki sehemu zingine wamemwagwa na sasa wanatumia nafasi ya LIGI YA USAJILI wa Dirisha Dogo watokee kupitia Lindi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2013

    Wadau wazo hili vipi?

    Kwa nini Mashindano ya Ulimbwende yasihusishe uwezo wa Washiriki ktk ujuzi wa Mapishi?

    Waulizwe Miss Tanzania,

    Maana sehemu yanakopita mashindano kila mahala wana uwezo wao na aina zao za lishe na kama mjuavyo watu tunapishana zaidi ya mambo mengi ya Warembo wavyo jisasambua na wanavyo tuwekea Jamvini siku za Mashindano sisi wengine ni Wapenzi wa MADIKO DIKO na MAHANJUMATI!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...