Muuguzi  wa  Taasisi ya Saratani  ya Ocean Road  (ORCI) Sr.  Felista John (katikati aliyevaa gauni jeupe) akipokea msaada wa vyakula mbalimbali  kutoka Meneja Uendeshaji Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mwanaisha Ayosi, iliyotolewa na benki hiyo kitengo cha Operesheni ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo. Wengine ni wafanyakazi katika kitengo hicho.
Mmoja wa wafanyakazi wa maofisa wa benki ya NBC, Lioba Massao (kushoto) akifanya maombezi kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya  Taasisi ya Saratani ya Ocean Road  (ORCI) katika hafla ambayo benki hiyo kitengo cha operesheni kilikabidhi  msaada wa vyakula mbalimbali ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii hospitalini hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo na pia kumkabidhi msaada wa sabuni ya kufulia.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC wakibeba mizigo ya vyakula na mafuta ya kupikia tayari kuwakabidhi wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam kama sehemu ya juhudi za NBC katika kusaidia shughuli za jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2013

    Mungu awabariki sana hawa wafanyakazi wa NBC, niliwahi kuuguza binamu yangu pale OCEAN ROAD kwa kweli pale pana magumu na machungu kwa wagonjwa wa pale, maana wengi wao ni wa hali ya chini na mbaya zaidi wengi wanatokea mikoa ya mbali, hivyo wanakuwa hawana ndugu wa kuwasaidia zaidi ya kutegemea tu chakula cha pale hospitali na wasamaria wema watako tokea pale.

    Nashauri jamii nzima itambue hili na pale panapo kuwa najinsi ya kuwasaidia wasisite kutoa misaada yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...