Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kupitia Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA-ISP) imekabidhi vitabu vinavyohusiana na Taarifa za Hali ya Mazingira na Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Vyuo Vikuu mbalimbali hapa nchini.
Vitabu hivi ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira katika kujenga uwezo kwa wadau kuweza kuelewa na kutunza mazingira. Ofisi kwa kupitia programu hii itaendelea kushiriana na wadau mbalimbali kuelimisha umma dhana zima ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira hapa nchini.
Mratibu
wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi
ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kushoto) akikabidhi sehemu ya vitabu hivyo
kwa Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Misitu na Uhifadhi ya Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine Prof. Yonika M. Nganga.
Mratibu wa Programu ya Utekelezaji wa
Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi ya Makamu wa Rais, ndugu
Joseph Kihaule (kushoto) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dodoma, Prof. Idrisa Kikula (katikati), kulia ni Prof. Kinabo
akishuhudia.
Mratibu
wa Programu ya Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMAISP), Ofisi
ya Makamu wa Rais, ndugu Joseph Kihaule (kulia) akikabidhi baadhi ya vitabu kwa
Naibu Mrajisi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijini cha Dodoma, Prof.
Innocent J.E Zilihona.
Hapa akikabidhi baadhi ya vitabu hivyo kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Mafunzo, ndugu Edwin
Lyanda wa Chuo Kikuu cha Mkwawa, Iringa. Aidha vitabu vingine vilikabidhiwa
kwa Vyuo Vikuu vya St. John’s, Dodoma, Chuo Kikuu cha Kiislamu, Morogoro na
Chuo Kikuu cha St. Augustine Tawi la Morogoro (Jordan University)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...