Afisa wa Mfuko wa Pspf Mkoa wa Lindi Bw Delphil Richard
Akibainisha mafao yanayotolewa na PSPF.
Walimu Tarajari Chuo cha Ualimu Nachingwea wakipata somo
kuhusiana na Mfuko wa PSPF unavyohudumia wanachama wake.
Na Abdulaziz Video
Walimu tarajiwa katika chuo cha Ualimu Nachingwea mkoani Lindi
wameshauriwa kujiunga na mfuko wa penseni kwa watumishi wa umma
Pindi wamalizapo mafunzo yao na kupata ajira.
Wito huo umetolewa na Afisa wa Mfuko wa Pspf Mkoa wa Lindi Bw Delphil
Richard alipokuwa anazungumza na wanachuo hao kwenye semina yakutoa
elimu kuhusu mfuko huo kwa wananachama wake na walimu tarajari katika
chuo hicho.
Richard alisema kuwa lengo la kukutana na walimu hao watarajiwa ni
kuwahamasisha kujiunga na mfuko wa PSPF na kutoa taarifa mbalimbali
ikiwemo michango na usajili wa uanachama na kubainisha kuwa mfuko
unatoa mafao mbalimbali kwa wanachama wake yakiwemo ya uzeeni,
ulemavu, mirathi, rambirambi za mazishi, wategemezi, na malipo ya
pensheni ya kila mwezi.
Richard aliongeza kuwa pamoja na huduma hizo pia mfuko umeanzisha
mpango wa uchangiaji wa hiari kwa ajili ya kupanua wigo wa uanachama
kwa kuandikisha wananchi walioajiriwa au kujiajiri katika sekta rasmi
na isiyo rasmi.
Kupitia mpango huo utawezesha wale wote ambao hapo awali hawakuweza
kupata huduma ya hifadhi ya jamii kutokana na kutokuwa katika ajira
rasmi ambapo sasa kupitia mapato yake anao uwezo wa kujiunga na PSPF


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...