New Picture (9)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.

Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.

Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2013

    Mimi huwa nafurahia sana nchi ya uingereza wanaposaka mtu kama huyo .jeshi huwa linatangaza kuwa no a single stone will be left unturn na kweli unashangaa huyo ndani ya muda.na jeshi letu lijifunze kutangaza msimamo wa kutafuta waharifu kama hao ili kuonyesha commitment yao. tunatarajia watamkamata tu mshenzi huyo.nchi yetu taratibu mwendo wa kinyonga inabadirika.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2013

    Poleni ndugu zangu wote, hii ni hali ya hatari.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 07, 2013

    Yes, upendo kwa wananchi wako ndio upendo kwetu kwako Mh Rais.

    Kata raha uje uungame karaha.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 07, 2013

    'Ameguswa'

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...