Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam kwa niaba ya Katibu mkuu Kiongozi
kuhusu Hali ya Lishe nchini , mkakati wa serikali katika kuhakikisha
kuwa wananchi wanapata virutubisho muhimu kupitia vyakula na Kampeni ya
uhamasishaji wa matumizi ya Lishe bora nchini itakayozinduliwa
tarehe 16 mwezi huu na Rais Jakaya Kikwete katika viwanja vya Mnazi
mmoja jijini Dar es salaam yakiongozwa na kauli mbiu "Lishe bora ni Msingi wa Maendeleo ,Timiza wajibu wako".
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula la Lishe Tanzania
Faith Magambo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu madhara
yanayosababishwa na ukosefu wa lishe kwa watoto na umuhimu wa maziwa ya
mama katika kujenga afya bora ya mtoto. Kulia ni Katibu mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu Peniel Lyimo.
Katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Peniel Lyimo akipokea
na kujibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi
wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es salaam.
Waandishi wa Habari wakiwa Kazini wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...