HATIMAYE katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na
wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili.
Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka
shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu
na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo
alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa
kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa
imegundua kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala
ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana
na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi
yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba
watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu
kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni
yaliyokusudiwa.
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu. |
Kila la kheri;cha msingi tu haki itendeke kwa kila raia. Ardhi ilitolewa kwa matumizi ya ujenzi wa chuo kikuu(elimu).Sasa anayeuza anakiuka sheria za wakfu. Tujitahidi kutenda uadilifu.
ReplyDeleteAliyandika hii story amesimuliwa au? Mara ponda ameshinda mashitaka yote yaliyokuwa yakimkabili... hapo hapo amehukumiwa kifungo...mara jaji aliyesoma hukumu n.k.
ReplyDeleteUnajua kweli unaripoti nini au haraka ya kupost story?
Kikubwa ni haki kutendeka na tunashukuru kwa hilo.
ReplyDelete