Kama ni mpitaji mzuri wa barabara Kawawa jijini Dar,basi ni lazima utakuwa umekutana na hadha ya shimo hili lililopo pale Kinondoni Mkwajuni.Kiukweli shimo hilo ambalo ni la kudumu,limekuwa ni kero kubwa sana kwa watumiaji wa njia hiyo hasa kwa wenye magari madogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    Yaani hata Meya wa Kinondoni anapita hapo hapo lakini nashangaa kuwa shimo limedumu zaidi ya mwaka mmoja!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2013

    Hata sielewi watu wanalipa road tax ya kitu gani Mie nalaumu makampuni ya wanopewa kutengeneza barabara ni matapeli wakubwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2013

    Jamani TZ tunapiga hatua, tumeacha kulalamika barabara zenye lami mbovu miaka kadhaa iliopita sasa tupo kwenye kulalamika shimoz hapa na pale - ni uzuri sana kuwanyooshea vidole wahusika lakini tusisahau tu kuwa Rome was not build in one day....tuna safari ndefu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2013

    Sio mwaka mmoja tu mimi naishi mita 50 kutoka hapo ,hilo shimo lilikuwepo hapo tangu mwaka 2010 na huyu meya wetu mpaka majuzi alipita hapo gari lake likawa limesimamama lumpisha dereva nwingine apite kwamza, lakini labda alikuwa kapiga usingizi hajaliona

    ReplyDelete
  5. Ndugu,

    Kwanza nimpongeze huyu aliyepiga hii picha. Kuna watu wapuuzi sana , wanakaa hata hawafikiri kitu kimoja labda mpaka muheshimiwa rahisi azungumze ili hili shimo lizibwe haraka sana. nimeshaona karibu ajali nne zitokee hapa, watu kukwaruzana na ukipita hapa kwenye shimo kwa speed ndogo kiasi unaweza ukaacha tairi. Hivi hii mianaume iliyoko kwenye hili eneo wanafanya nini miaka zaidi ya 2 sasa. si kumlaumu contractor kwani barabara iko safi kabisa ni kasehemu hapo kadogo tu, kana kaa miaka. Kuna watu wenginae hawafikiri zaidi ya mitumbo yao tu. Yaani nimechukizwa ni huu upuuzi wa kukaa ofisini halafu mali za watu zinaharibika. kuna kuna gharama gani kutengeneza hapa. hili ni suala la kutazamwa na meya au mtu mhusika kutafuta lami na kuziba hapo? inatia aibu sana, mkurungenzi haoni hili kweli, diwani, meya, mkuu wa mkoa kitu kidogo namna hii ? Naomba watu wawajibike katika hili.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2013

    Watu wengine yameshikilia ofisi bila hata kuona aibu? hivi hili shimo linaitaji mtaalamu kutoka nje? Hakuna dereva anayepita hii barabara asiyejua hili shimo na kero yake. Saa nyingine linasababisha foleni kubwa sana. Lakini wahusika sijui wako nchi gani, wao ni kuangalia maslai yao tu.

    Huu ni upuuzi na uzembe wa kupindukia

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2013

    Ningekuwa mimi ndiye Afisa mtendaji wa eneo hili ningemtonya Katibu Tarafa na diwani faster tukaweka mawe na kokoto angalau kunusuru wapitaji na magari yao tukisubiri matengenezo makubwa kwa mujibu wa mipango ya LGA

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2013

    hili shimo nomaaa. kama shimo la taka vile manake ni kubwa sana. ukipita na gari ndogo unaweza ukalia manake linazama lote kwa mbele afu kutoka ndo shughuli. utatamani kulia kwajinsi gari lako linavyoumia. clouds fm waliripoti lakini mpaka sasa hakuna kitu kimefanyina. hilo shomo liko hapo toka 2010 hadi leo. mvua ikinyesha ndio balaa. hapo lilipo ni afadhali manake baada ya mvua kukatika wasamaria walijaza michanga usiombe mvua unyeshe. MDAU WA MKWAJUNI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...