Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi akiongoza Kikao na Wawakilishi wa Nchi za Umoja wa Ulaya waliomtembelea Wizarani. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Said Mwema pia alihudhuria Kikao hicho akiwa na Wakuu wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam (Kushoto).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza na mmojawapo wa Wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya waliofanya kikao naye jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Said Mwema. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel nchimbi amesema Serikali imeimarisha shughuli za ulinzi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa wananchi na wageni wanaishi na kufanya shughuli zao kwa amani. 

 Dk. Nchimbi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Ujumbe wa wawakilishi wa nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na baadhi ya mabalozi wa Nchi hizo waliopo hapa nchini. 

 Aliuambia ujumbe huo ulioongozwa na Balozi Filberto Cerani Sebregondi kuwa Jeshi la Polisi limeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu katika jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi.

 Amesema kwa upande wa raia wa kigeni, Jeshi hilo limeanzisha Dawati Maalumu litakalohudumia raia hao pale wanapopata matatizo ili waweze kupata huduma za haraka.

 Kwa upande wake, Kiongozi wa Ujumbe huo amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na ameishukuru Wizara hiyo kwa jitihada inazoendelea kuchukua kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa wageni na raia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2013

    tunasema tumejitawala mbona kila kitu mpaka tukaripoti kwa EU na wamarekani na kujipendekezesha kwao? jee huu ndio uhuru ? au ukoloni mamboleo bado unaendelea , tunatawaliwa indirectly na hawa pampja na akina UN , harambeeeeeeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...