Familia ya Bernard Thomas Nderumaki (Mzee NDE) wa Kijitonyama, Dar es Salaam tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika msiba wa Baba yetu mpendwa ambaye alifariki tarehe 10 April, 2013 katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kuzikwa nyumbani Kilema, Moshi tarehe 15 April, 2013.
Shukrani zetu za dhati ziwaendee Madaktari wa Hospitali ya Mwananyamala, Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Paroko, Mapadre na masista wa Kanisa Katoliki Mwananyamala na Masista kutoka Dodoma, Jumuiya ya Mt. Clara na Kanda ya Makumbusho, Paroko na Mapadre wa Kanisa Katoliki la Maua, Kilema, Jumuiya ya Mt. Yakobo Mtume Kilema, Majirani wote, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Dar es Salaam, Moshi, Arusha na Shinyanga.
Kwa vile si rahisi kumtaja kila mmoja peke yake, tunaomba mzipokee shukrani zetu za dhati na tunasema Ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu na Mungu awabariki.
Raha ya milele umpe eeh Bwana na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani.
Amina.
“Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe” AYU 1:21
Mungu amlaze mahali pema peponi mzee Ndee.Poleni sana ndugu zangu. wenu Mike.
ReplyDelete