Watanzania waishio New jersey na New York na kote kwingineko tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa ushirikiano wenu mkubwa mlio tuonyesha katika kipindi hiki kigumu. Kwa ajili ya blog za watanzania tuliweza kufikisha habari za msiba wa marehemu Adolf aka Brian aka Thadeo Lwakajende kwa watu wengi sana kwa muda mfupi sana kuliko tulivyotegemea. Kwa ushirikiano wenu huo tuliweza kufanikiwa na kuweza kukamilisha shughuli hii kwa kipindi kifupi sana kuliko tulivyokua tunafikiria.
Adolf alipelekwa kulazwa katika nyumba yake ya milele jana Jumatano May 1st, 2013 huko katika makaburi ya Mt Pleasant, Hawthorne, NY 10532.
Tunashukuru sana sana kwa ushirikiano wenu mliotuonyesha na pia niwaombe radhi wale walioniandikia lakini sikuweza kuwajibu email zao.
Asanteni sana,
Pauline
RIP. Maisha lazima yaendelee, sasa hiyo mashine ya kuzikia si mletage na huku jamani. Kuzika kwa mitulinga karne hii si vema jamani.
ReplyDeleteWATANZANIA TUJIFUNZE KUWEKA AHADI KWAMBA MAZIKO SAA FULANI BASI TUWEPO SIYO ETI LEO TUNAAMBIWA SAA FULANI AHALFU INACHUKUA LISAA LIMOJA AU LIMOJA NA NUSU NDO MNAAZA MISAA TUPO MAJU LAKINI BADO HATUBADILIKI NA ZA KIBONGO BONGO
ReplyDelete