MAREHEMU MZEE JAMES GERALD MANDAWA

Familia ya Marehemu Mzee James Gerald Mandawa wa Kiwalani, Dar es salaam, inapenda kutoa shukurani za dhati kwenu wote mlioshiriki kwa moyo wa upendo katika kufanikisha shughuli za msiba wa Mzee wetu Mpendwa James Gerald Mandawa.
Tunawashukuru sana kwa faraja na ushirikiano mkubwa mliotupatia katika kipindi hiki kigumu sana cha kuondokewa na Baba yetu Mpenzi, ambaye tulimpumzisha katika nyumba yake ya milele huko shambani kwake Kiluvya, Dar es salaam.
Shukurani ziwafikie Madaktari na wauguzi wa hospitali ya Hindu Mandal, na hasa Dkt R. Kaushik , Menejimenti na wafanyakazi wa TASAF Makao Makuu,Uongozi na wafanyakazi wa PRIDE –Arusha, Uongozi na wafanyakazi wa DAWASCO Ilala    Uongozi, wana jumuia na kwaya ya kanisa la Kianglikana, Mt. Thomas –Yombo, majirani na marafiki wote.
Ni vigumu kuwataja wote, lakini tunawaomba wote mpokee shukurani hizi kwa moyo mkunjufu.
Baba, tulikupenda sana, kuondoka kwako kumekuwa ghafla sana, lakini tunamshukuru Mungu kwa yote”.
Familia inapenda kuwataarifu na kuwaomba mshiriki  pamoja nasi kwenye mkesha wa kumaliza msiba, tarehe 24 kuamkia 25 Mei, 2013- Kiwalani, na kwenye misa ya shukurani itakayofanyika siku ya jumamosi tarehe 25 Mei, 2013 saa mbili asubuhi, kwenye kanisa la Mt. Thomas, Yombo-Kiwalani, DSM.
BWANA  ALITOA, BWANA AMETWAA, 
JINA LAKE LIHIMIDIWE
AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2013

    poleni sana familia ya mzee mandawa kwa kuondokewa na mzee wetu, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!!!!

    magambo from canada!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 18, 2013

    jamani huyu mzee ndiye yule aliyewahi kufanyia ALAF na UNILEVER...

    poleni wanafamilia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...