KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA BI JOYCE K.G. MAPUNJO
ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTUMISHI WAKE, NDUGU ELIAS DANIEL KITUNDU
KILICHOTOKEA ALFAJIRI YA LEO TAREHE 27 MEI 2013 KWA AJALI YA KUGONGWA NA TRENI, UKONGA DSM.
MIPANGO YA MAZISHI INAFANYWA NYUMBANI KWA MAREHEMU NA TAARIFA ZAIDI KUHUSU MSIBA HUU ZITATOLEWA BAADAE
HABARI ZIWAFIKIE, WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA MH DKT ABDALLAH KIGODA NA NAIBU WAKE MH GREGORY TEU WA BUNGENI DODOMA
VIONGOZI NA WAFANYAKAZI WOTE WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA NA TAASISI ZAKE ZOTE POPOTE WALIPO
WADAU WA SEKTA NDOGO YA NGOZI KOTE NCHINI,
WAZAZI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU POPOTE WALIPO.
MUMGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI,
AMINA.
HII NDIO GARI ALIYOPATA NAYO AJALI,NDUGU ELIAS DANIEL KITUNDU.
RIP marehemu na poleni sana familia.
ReplyDeleteMichu lugha aliyotumia katibu mkuu si sahihi kusema mtumishi wake..usahihi ni mtumishi wa wizara.. maana wizara si mali au kampuni binafsi ya katibu mkuu!
nawasilisha
mdau
j4
ujerumani
juzi nimekoswa koswa na treni asubui, wale washika kibendera wafukuzwe kazi waletwe watu wenye akili imagine amekaa chini ya mtu na kibendera alfajiri huku train inakuja!! badala aonyeshe ishara ili watu tujue train inakuja yaani sitaki kukumbuka sasahivi mama yangu angekuwa analia msiba.
ReplyDelete