Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania, Phocus Lasway (kulia) akikabidhi vazi la suti mpya maalum kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah wakati wa hafla maalumu ya kuonesha vazi hilo la suti mbele ya wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo,iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar. Wa pili kulia Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wakipita jukwaani huku wakiwa wamevalia suti hizo wakati wa hafla maalum ya kuonyesha mavazi yao hayo iliyofanyika jana jioni Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.
Wachezaji wa Taifa Stars, benchi la ufundi na maofisa wakuu wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuonesha suti mpya
Wachezaji wa Taifa Stars na benchi la ufundi katika picha ya pamoja.
Wadau wa soka nchini wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi suti mpya kwa Taifa Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2013

    Hongera sana kwa Mdhamini
    Hivi ndivyo ilivyotakiwa waende Ikulu wakiwa wamevaa Suit na sio yale mabango

    Ninachoomba ni kuwa tuwe na usimamizi wa jinsi gani ya kuvaa maana wachezaji wetu wengi hawavaagi suit mara kwa mara

    Hivyo si ajabu ukakuta hawajavaa tai au wameregeza tai au hata hawajachomekea shati na uvaaji mwingine wowote ambao si wa suit

    Hongereni sana wadhamini na TFF kwa ujumla

    Mdau
    Maseru, Lesotho

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2013

    Nimeipenda hii ya Taifa Stars kuvaa suti wanapotuwakilisha kwenye mashindano ya kimataifa. Nchi yetu ina ma-designer wa nguo wazuri kama akina Sheria Ngowi, nategemea watakuwa wameungwa mkono badala ya kuagiza suti kutoka nje ya nchi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2013

    kusema ukweli wamependeza.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2013

    Suti zimewakubali.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2013

    duuh safi sana, aliyewadizainia ndo huyo sheria? utafikiri wachezaji wa mbelembele lol..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2013

    Tunaomba picha upclose za hizi suti

    Pia tunataka kujua kama local designers wamewezeshwa au vipi?

    Niliona design concepts za Sheria Ngowi kwa Taifa stars kwa kweli niliridhika lakini tunahitaji kuona zaidi maana sie wabongo kwa mambo ya kuunganisha unganisha ndio wenyewe, Standards zetu always ni zero...isije kuwa mtu kapewa tenda kisha anaenda kuzifyatua tuu huko china

    natumaini designers wazalendo kama akina mustafa hassanali, Mwanamboka, Ally Rehmtullah nao walipewa nafasi na ingependeza kujua mchakato ulienda vipi?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2013

    hawa wachezaji wataanza kuvaa milegezo nyie mtaona tu! watu wa tbl muwe makini kuhakikisha wanavaa inavotakiwa, suti ni nzuri sana

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2013

    hiyo kazi ya kutengeneza suti hao kina mwanamboka hawawezi, ila sheria ndo mwake humo, i knw the guy, nimesoma nae na i remember toka alivoanza kutengeneza hizo suti.. so gud choice kw tbl kumchagua sheria adesign.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...