Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania, Phocus Lasway (kulia) akikabidhi vazi la suti mpya maalum kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah wakati wa hafla maalumu ya kuonesha vazi hilo la suti mbele ya wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo,iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar. Wa pili kulia Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.

Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wakipita jukwaani huku wakiwa wamevalia suti hizo wakati wa hafla maalum ya kuonyesha mavazi yao hayo iliyofanyika jana jioni Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.
Wachezaji wa Taifa Stars, benchi la ufundi na maofisa wakuu wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuonesha suti mpya
Wachezaji wa Taifa Stars na benchi la ufundi katika picha ya pamoja.
Wadau wa soka nchini wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi suti mpya kwa Taifa Stars.
Hongera sana kwa Mdhamini
ReplyDeleteHivi ndivyo ilivyotakiwa waende Ikulu wakiwa wamevaa Suit na sio yale mabango
Ninachoomba ni kuwa tuwe na usimamizi wa jinsi gani ya kuvaa maana wachezaji wetu wengi hawavaagi suit mara kwa mara
Hivyo si ajabu ukakuta hawajavaa tai au wameregeza tai au hata hawajachomekea shati na uvaaji mwingine wowote ambao si wa suit
Hongereni sana wadhamini na TFF kwa ujumla
Mdau
Maseru, Lesotho
Nimeipenda hii ya Taifa Stars kuvaa suti wanapotuwakilisha kwenye mashindano ya kimataifa. Nchi yetu ina ma-designer wa nguo wazuri kama akina Sheria Ngowi, nategemea watakuwa wameungwa mkono badala ya kuagiza suti kutoka nje ya nchi.
ReplyDeletekusema ukweli wamependeza.
ReplyDeleteSuti zimewakubali.
ReplyDeleteduuh safi sana, aliyewadizainia ndo huyo sheria? utafikiri wachezaji wa mbelembele lol..
ReplyDeleteTunaomba picha upclose za hizi suti
ReplyDeletePia tunataka kujua kama local designers wamewezeshwa au vipi?
Niliona design concepts za Sheria Ngowi kwa Taifa stars kwa kweli niliridhika lakini tunahitaji kuona zaidi maana sie wabongo kwa mambo ya kuunganisha unganisha ndio wenyewe, Standards zetu always ni zero...isije kuwa mtu kapewa tenda kisha anaenda kuzifyatua tuu huko china
natumaini designers wazalendo kama akina mustafa hassanali, Mwanamboka, Ally Rehmtullah nao walipewa nafasi na ingependeza kujua mchakato ulienda vipi?
hawa wachezaji wataanza kuvaa milegezo nyie mtaona tu! watu wa tbl muwe makini kuhakikisha wanavaa inavotakiwa, suti ni nzuri sana
ReplyDeletehiyo kazi ya kutengeneza suti hao kina mwanamboka hawawezi, ila sheria ndo mwake humo, i knw the guy, nimesoma nae na i remember toka alivoanza kutengeneza hizo suti.. so gud choice kw tbl kumchagua sheria adesign.
ReplyDelete